UTARATIBU UNAOTUMIKA KUTOA VIBALI VYA UJENZI WA MAJENGO :-
1. KIBALI CHA UJENZI
Kulingana na Sheria ya Serikali za Mitaa Na. 8 ya mwaka 1982.
Sheria ya Mipango Miji na Majengo Mijini si ruhusa kwa mtu yeyote kujenga au kuanza kujenga jengo bila:-
i.Kutuma maombi kwa mamlaka ya Mji kwa kupata ridhaa ya awali (Planning Consent)
ii. Majengo makubwa kuwe na ramani (Outline scheme designs)
iii.Kuwasilisha michoro ya jengo na kumbukumbu husika za kiwanja.
iv.Kupata kibali kwa maandishi kinachoitwa “Kibali cha Ujenzi”.
2. KIBALI CHA AWALI (Planning Consent);
Inashauriwa kupata kibali cha awali kabla ya kuomba kibali cha ujenzi. Hivyo muendelezaji anatakiwa aandae mchoro wa awali (Outline plan) kwa utaratibu unaotakiwa ukionyesha aina ya ujenzi atakaokusudia kufanya ili aweze kupata ridhaa ya kuendelea na hatua za kuandaa michoro ya mwisho.
FAIDA:
Kuokoa muda na gharama, iwapo michoro ya mwisho itaonekana kuwa na dosari za kitaalam ambazo zitahitaji kufanyiwa marekebisho.
Kuwa na uhakika kuhusu mahitaji muhimu ya kuzingatiwa wakati michoro inaandaliwa.
3. JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI YA KIBALI CHA UJENZI
Baada ya michoro kukamilika, iwasilishwe ikiwa kwenye majadala kwa namna ambayo inaweza kufunguliwa na kusomeka. Michoro hiyo iwasilishwe kama ifuatavyo:-
Seti tatu za michoro ya jengo (Architectural drawings)
Seti mbili za michoro ya vyuma) structural drawings) kwa majengo ya ghorofa.
4. MICHORO ILIYOANDALIWA IONYESHE NINI
Michoro itakayoandaliwa inatakiwa ionyeshe mambo yafuatayo:-
Jengo litakavyokuwa (Plan) Sections, elevations, Foundation and roof Plan).
Namba ya eneo la kiwanja kilipo,Jina la Kampuni na anwani ya Kampuni iliosanifu jengo husika.
Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba
2
Ujazo wa kiwanja (Plot coverage)
Uwiano(Plot ratio)
Urefu wa jengo (height)
Matumizi yanayokusudiwa Idadi ya maegesho yatakayokuwepo
Umbali wa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja (setbacks) na
Mfumo wa kutoa maji taka hadi kwenye mashimo. Barabara inayopitia mbele ya kiwanja na mshale unaoonyesha Kaskazini.
5. VIAMBATANISHO
Fomu moja ya maombi iliyojazwa kwa usahihi.
Hati ya kumiliki kiwanja au barua ya toleo au leseni ya Makazi
Kumbukumbu nyingine zinazohusu kiwanja hicho kama hati za mauzo, makabidhiano n.k.
Nakala za risiti ya kodi ya kiwanja na kodi ya majengo
Mabadiliko ya matumizi ya ardhi.
6. HATUA ZINAZOFUATWA KATIKA KUSHUGHULIKIA MAOMBI YA KIBALI
Zifuatazo ni hatua zinazofuatwa wakati wa kuchunguza michoro hiyo:-
Kuwasilisha michoro na kulipa gharama za uchunguzi(scrutiny fee).
Uhakiki wa miliki
Kukaguliwa usanifu wa michoro
Kukaguliwa kiwanja kinachokusudiwa kuendelezwa
Uchunguzi wa upimaji kiwanja
Uchunguzi wa matumizi ya jengo na uwiano
Uchunguzi wa Maafisa Afya
Uchunguzi wa Mipango ya uondoaji majitaka
Uchunguzi wa tahadhali za moto
Uchunguzi wa athari za mazingira (EIA)
Uchunguzi wa uimara wa jengo (Structural Drawings)
Kuandaliwa kwa maombi yaliokamilisha taratibu hizi na kupelekwa kwenye Kamati ya Ujenzi ambayo wajumbe wake ni Madiwani
Hatimaye kuandika na kutoa kibali
7. FAIDA ZA KUJENGA NYUMBA IKIWA NA KIBALI CHA UJENZI
Kuishi kwenye nyumba ambayo imethibitishwa kitaalamu kuwa ni salama
Kuwa na mazingira bora kwa kuwa na mji ulipangwa
Kuepuka hasara na usumbufu unaoweza kutokea iwapo ujenzi umefanyika bila kibali kiwa ni pamoja na kushitakiwa mahakakani, kuvunjiwa na kulipa gharama za uvunjaji.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa