TARATIBU ZA UTOAJI LESENI ZA BIASHARA
Mteja kujaza fomu ya Maombi ya Leseni za biashara TFN 211 FOMU YA BIASHARA.pdf na kuambatisha nyaraka zifuatazo:-
(Photocopy of Certificate of Incorporation or Registration & Extract);
ambazo zitaonyesha kuwa Kampuni imeruhusiwa Kisheria kufanya biasharainayoombwa, pamoja na Majina ya Wamiliki wa kampuni, hisa zao na Utaifa wao;
Pamoja na hati ya udhibitisho kuwa hadaiwi kodi ( BusinessLicense Tax Clearance certificate)
Mfano wa Taasisi / Mamlaka za Udhibiti wa biashara za Kisekta
TFDA –
Leseni zote zinazohusu usindikaji / ufakataji wa vyakula, Uuzaji wa madawa.
CRB -
Leseni ya ukandarasi wa majengo na barabara. Nk.
Hati ya utaalam (Professional certificates)
– Kwa biashara zote za kitaalam – mfano leseni za kuendesha hospitali, zahanati,udaktari, sheria, uhandisi, urubani wa ndege, unahodha wa meli n.k.
Kulipia ada za Leseni
Baada ya kuwasilishwa kwa fomu na viambatisho vyake, Afisa biashara humwandikia kiwango cha Ada kinachotakiwa kwa kutumia mfumo waukadiriaji na malipo wa LGRCIS (Kwa kuzingatia orodha iliyopo kwenye Schedule
ya Ada za Leseni) Kisha Mteja atakwenda Benki/Dawati la malipo kulipa ada husika na kupata stakabadhi ya malipo halali,
A. MAOMBI YA LESENI MPYA.
Kwa mteja anayehuisha Leseni, ni kwamba Afisa wa Leseni anataarifa za mteja huyo kwa kuwa alizihitaji wakati wa kutoa Leseni mara ya kwanza.Kwa hiyo taratibu za kufuata ni:-
1. Kujaza fomu ya maombi ya Leseni na kuambatisha nyaraka zifuatazo:-
Kulipia ada za Leseni
Mteja anapaswa kujaza fomu kwa ufasaha na kuweka viambatisho vyake, kisha kuiwasilishara kwenye dawati la ukadiriaji, ambapo Afisa biashara husika humkadiria kiwango cha Ada kinachotakiwa kwa kutumia mfumo wa ukadiriaji na malipo wa LGRCIS (Kwa kuzingatia orodha iliyopo kwenye Schedule ya Ada za Leseni) Kisha Mteja atakwenda kwenye tawi lolote la benk ya NMB kulipa ada husika na kupata hati ya malipo ya benk ambayo ataiwasilisha katika dawati la malipo la Halmashauri na atapatiwa stakabadhi ya malipo. Bofya
Kuandikwa na kusainiwa leseni
Baada ya kukamilisha malipo, hatua inayofuata ni kuadikwa na kusaini kwa leseni; mteja anawasilisha maombi yake yakiambatana na stakabadhi ya malipo kwenye dawati la usajili.
Bofya hapa ili uweze kupakua Fomu ya Leseni ya Biashara.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa