Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Kihongosi Leo amekabidhi HATI za Vijiji 25 za Wilaya ya Tatu za Mkoa wa Simiyu baadha Kukamilika kwa Mradi wa UPIMAJI Ardhi katika Vijiji 25 vilivyopo kando ya Hifadhi ya Poli la Akiba la Maswa.
Zoezi Hilo lililo ratibiwa na na Serikali kupitia Mamlaka ya Upangaji wa Ardhi Kwa kushirikia na Mamlaka za Serikali za Mitaa za Halmashauri Tatu kwa ufadhili wa Shirika La Frankfurt Zoology Society la Ujerumani.
Akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mradi kwa niaba ya Mkurugenzi Tume ya Taifa ya mipango ya matumizi ya Ardhi Ndg. Jonas Masingija.
"Tume ya Taifa ya mipango ya Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na Mamlaka za Up, hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Shirika La Frankfurt Zoological Society kwa pamoja kwa kushirikiana naamlaka za Upangaji za Wilaya ya Meatu, Itilima na Busega tuliweza kutekeleza Mradi wa dharula wa wa Uhifadhi wa Bayonuai.
Lengo kuu la Mradi ni kuleta hauweni kwenye madhhara ya Uviko -19"
Mradi huu umetekelezwa katika Vijiji 25 vya Halmashauri Tatu kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Mradi umepima Vijiji 9, Meatu 12 na Busega Vijiji 4.
Utekelezaji wa Mradi huu kwanza ulihusisha utatuzi wa Migogoro ya Mipaka, uhuishaji na Upimaji wa Mipaka ya Vijiji, utoaji wa Mafunzo na Elimu kwa Umma na uandaaji wa matumizi ya Ardhi katika Vijiji vya Mradi.
Awamu ya pili ya utekelezaji wa Mradi ulihusisha uandaaji wa vyeti vya Vijiji uhakiki vipnde vya Ardhi Kwa mawanchi Mmoja Mmoja, uandaaji wa Mpango kina na utaarishaji wa HATI miliki za kimila kwa Wananchi ambao maeneo Yao yalikuwa yametambuliwa
Aidha Ndg. Jonas Masingija alisema kuwa Mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020/2025 ambayo imeelezewa katika ibara ya 69 ambayo inaeleza kuwajengea uwezo Mamlaka za hifadhi katika kutatua migogoro baina ya Wananchi na Maeneo yaliyo hifadhiwa.
Katika makabiziano hayo ya hati Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Kihongosi alisema
"Niwapongeze sana Mamlaka husika na kipekee Mtakuwa mme wawezesha Wananchi kumiliki Ardhi Kisheria na hata kuwasaidia kukopesheka katika Taasisi za Fedha.
Kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu D. Silanga (Mb) aliishukuru Mamlaka zilizo tekeleza Mradi huu na hatimaye Upimaji wa Vijiji 26 vya Wilaya ya Meatu, Busega na Itilima Kukamilika ni faraja ya kipekee na ni ahadi ya Ilani ya Chama chetu tuliyo waahidi Wananchi wetu ili kutanzua migogoro iliyo kuwepo baina ya Wananchi na Mamlaka za Uhifadhi.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Anna Gidarya alitoa Rai kwa Viongozi wa Serikali za Vijiji kuwa kwa Upimaji huu kusiwepo na Changamoto ya uchukiaji wa maeneo kiholela kwa tumeshatoka huko Vijiji vimepimwa na vina HATI na Wananchi wana HATI za Maeneo Yao.
Aidha Mhe. Gidarya alimuomba mhe. Kihongosi kuwasilisha Shukrani za Wanaitilima kwa Mhe. RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha Mradi huu wa Kipekee kwa Wananchi wa Wilaya hizi tatu na wenye Gharama Kubwa.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa