• MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
Itilima District Council
Itilima District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Sisi ni nani?
    • Dira na Dhamira
    • Taarifa ya Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango
      • Afya
      • Mifugo
      • Kilimo
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi
      • Sheria
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
    • Muundo
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Ujenzi
    • Leseni za Biashara
    • Umilikaji wa Ardhi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba Video
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi inayofadhiliwa na Wahisani
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea na Ujenzi
    • Maandiko ya Miradi
  • Zabuni
  • Uwekezaji
  • FFARS LINK

Mipango

IDARA YA MIPANGO, TAKWIMU NA UFUATILIAJI

Idara ya  Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji inashughulikia upangaji na uratibu wa mipango ya maendeleo katika miaka husika,  usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ya Halmashauri, Tafiti na ukusanyaji wa Takwimu pamoja na kuratibu shughuli za Uwekezaji.  Idara hii inaongozwa na Mchumi wa Manispaa na imegawanyika katika sehemu tano kama ifuatavyo:-

Ø  Mipango na Sera

Ø  Usimamizi na Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo

Ø  Uwekezaji

Ø  Tafiti na Takwimu.

Ø  Sehemu ya TASAF

  Sehemu ya Mipango na Sera.

Majukumu ya sehemu hii ni kama ifuatavyo:-

Ø  Kusimamia Uandaaji wa mpango wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kila mwaka.

Ø  Kuratibu ufanisi wa mifuko ya Halmashauri: LGCDG, Mfuko wa Jimbo na fedha za mapato ya ndani.

Ø  Uratibu na utayarishaji wa Mipango shirikishi katika Kata zote za Halmashauri kupitia Mfumo wa O&OD.

Ø  Uratibu na utayarishaji wa Mpango na Bajeti ya kila mwaka ya Halmashauri.

Ø  Kusimamia uandaaji wa mipango kazi (Action Plans) ya bajeti za kila mwaka na kuziwasilisha katika ngazi husika..

Ø  Kuratibu uandaaji wa maandiko ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ø  Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN)

Ø  Kuratibu maandalizi ya Sera na Mpango Mkakati wa Halmashauri

Ø  Kuratibu uandaaji wa taarifa mbalimbali za Halmashauri pamoja na taarifa za utekelezaji wa maagizo kutoka mamlaka za juu za serikali

Sehemu ya Usimamizi, Ufuatiliaji na Tathmini ya miradi ya

maendeleo.

Majukumu ya sehemu hii yapo kama ifuatavyo:-

Ø  Kuratibu uandaaji wa taarifa za Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya  2015 - 2020

Ø  Kufuatilia utekelezaji halisi na matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo.

Ø  Kuratibu miradi ya jumuiya za wananchi na taasisi nyinginezo za ndani na nje ikiwemo miradi ya wahisani

Ø  Kuratibu utekelezaji wa Mipango ya muda mrefu, kati  na mfupi ikiwepo Ilani ya Uchaguzi na uandaaji wa taarifa za utekelezaji wa mipango hiyo

Ø  Kuratibu utekelezaji wa mipango shirikishi.

Ø  Kuandaa taarifa za Miradi ya maendeleo ya Manispaa kwa vipindi mbalimbali na kuziwasilisha kwenye mamlaka husika.

Ø  Kuandaa mapitio ya bajeti ya kila mwaka baada ya kipindi cha nusu mwaka

Ø  Kuandaa mapendekezo ya kubadili matumizi ya vifungu vya bajeti ya maendeleo kila inapobidi.

Ø  Kuandaa taarifa za matukio ya kila wiki na kuiwasilisha ngazi ya mkoa.

Sehemu ya  Uwekezaji.

Sehemu hii hushughulikia mipango ya uwekezaji katika Halmashauri kwa kufanya yafuatayo:-

1. Kuratibu na kusimamia maandalizi ya mipango ya uwekezaji ya Halmashauri.

2. Kuratibu utekelezaji na uandaaji wa taarifa za mipango ya uwekezaji

3. Kuratibu utekelezaji wa miradi ya DMDP

Sehemu ya  Utafiti na Takwimu.

Sehemu hii hushughulikia masuala yanayohusu takwimu mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kuratibu shughuli za utafiti kama ifuatavyo:-

Ø  Kuratibu na kusimamia benki ya Takwimu ya Halmashauri ikihusisha takwimu za LGMD.

Ø   Kuhuisha na kuboresha Takwimu za Kiuchumi na Kijamii (Profile) za Halmashauri.

Ø  Kuratibu na kuhifadhi takwimu za Idadi ya watu za Halmashauri kwa

Ø  kutumia rejista za wakazi wa Mitaa.

Ø  Kuratibu na kutathmini utekelezaji wa Mpango mkakati wa Halmashauri 2012/13 – 2016/17

Ø  Kuratibu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.

Ø  Kuandaa taarifa za utatuzi wa kero na malalamiko kila wiki na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Mkoa

Sehemu ya TASAF

Utekelezaji wa shughuli za awamu ya tatu ya TASAF Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF III PSSN) katika Halmashauri ya wilaya ya Itilima uliendelea kama kawaida ambapo katika kipindi cha Januari hadi Machi, 2016 malipo kwa kaya maskini 6,262 kutoka katika mitaa 74 iliyopo kwenye mpango yalifanyika.

Vile vile Halmashauri imetoa mafunzo kwa wataalamu wa Elimu msingi, Elimu sekondari pamoja na Afya sambamba na kuendelea na zoezi la usambazaji wa fomu za kutimiza masharti ya elimu na afya kwa kuziwasilisha katika shule na zahanati za mitaa husika pamoja na kukusanya zile zilizosambazwa katika kipindi cha Novemba/Desemba.Vilevile madaftari pamoja na fomu za masharti ya elimu kwa shule zilizopo nje ya Halmashauri zimepangwa kulingana na wilaya/mkoa unaohusika na zimewasilishwa kwa mratibu wa mkoa kwa ajili ya ufuatiliaji.

Katika kipindi cha utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini cha kuanzia mwezi Januari hadi Machi, 2016 Halmashauri imeendelea na  utekelezaji wa zoezi la malipo ya Kaya Maskini ambapo shughuli zilizofanyika ni pamoja na malipo ya kaya maskini ya awamu ya tatu na awamu ya nne yaani malipo ya  mwezi Januari na Februari, 2016 (January/February Window Period) pamoja na malipo ya  mwezi Machi na Aprili, 2016 (Machi/Aprili Window Period). Katika kipindi cha malipo cha mwezi  Januari na Februari Halmashauri ilipokea kutoka TASAF  jumla ya sh. 301,243,500.00  ambapo kati ya fedha hizo fedha zilizokwenda katika ngazi ya jamii  kwa ajili ya malipo ya kaya maskini na asilimia ya mtaa ni sh. 272,336,295.45  na  sh. 28,907,204.55  zilizobaki katika ngazi ya Halmashauri kwa ajili ya uwezeshaji wa usimamizi na ufuatiliaji wa zoezi la malipo.  Vilevile katika kuongeza ufanisi wa ujazaji wa Fomu za Kutimiza mashrti ya Elimu na Afya Halmashauri imefanya mafunzo kwa wataalam mbalimbali wa ngazi ya kata wanaosaidia zoezi la malipo katika ngazi ya jamii na jumla ya wataalam 188 Walipatiwa mafunzo ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. Kati yao 110 ni waalimu wa shule za msingi, 51 ni walimu wa shule za sekondari na pia  wataalam wa Afya 27 wamepatiwa mafunzo. Katika kipindi cha malipo cha mwezi  Machi na Aprili Halmashauri ilipokea kutoka TASAF  jumla ya sh. 298,782,000.00  ambapo kati ya fedha hizo fedha zilizokwenda katika ngazi ya jamii  kwa ajili ya malipo ya kaya maskini na asilimia ya mtaa ni sh. 270,000,000.00  na  sh. 28,671,000.00  zilizobaki katika ngazi ya Halmashauri kwa ajili ya uwezeshaji wa usimamizi na ufuatiliaji wa zoezi la malipo. Aidha katika kuhakikisha Halmashauri inakuwa na taarifa sahihi za watoto wanaotakiwa  kutimiza mashrti ya Elimu na Afya waalimu na wataalam wa afya wa ngazi ya kata walishiriki zoezi la malipo kwa kuandikisha watoto kutoka katika familia za walengwa wa mpango ambapo jumla ya wataalam 101(waalimu 74  na watumishi wa afya 27) walishiriki zoezi hilo katika mitaa 74 iliyoko kwenye mpango. 

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA WILAYANI ITILIMA October 30, 2021
  • Tangazo Kwa Watumishi Wapya Wanao endelea kuwasili Wilayani Itilima July 03, 2022
  • "Tutaukaribisha Mwenge wa Uhuru Wilayani Itilima tarehe 9/7/2022 tutaupokea katika Viwanja vya Ushirika, Nyamalapa na mkesha utakuwa katika viwanja vya Halmashuri ya Wilaya ya Itilima Wananchi wote, Wafanyakazi tuungane katika makaribis July 07, 2022
  • "Tutaukaribisha Mwenge wa Uhuru Wilayani Itilima tarehe 9/7/2022 tutaupokea katika Viwanja vya Ushirika, Nyamalapa na mkesha utakuwa katika viwanja vya Halmashuri ya Wilaya ya Itilima Wananchi wote, tuungane katika kuukaribisha Mwenge July 06, 2022
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • TUME YA TAIFA YA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI YAPIMA NA KUKABIZI HATI ZA VIJIJI 25 VILIVYOPO KANDO YA POLI LA AKIBA LA MASWA

    June 30, 2024
  • BARAZA LA ARDHI ITILIMA SASA RASMI BAADA YA KUAPISHWA KWA WAJUMBE WA BARAZA

    June 26, 2024
  • KUNA MAISHA BAADA YA UTUMISHI WA UMMA

    June 20, 2024
  • MWALIMU TIMIZA WAJIBU WAKO WA MSINGI KWA AJILI YA NCHI YAKO, WAZAZI WA TANZANIA NA WATOTO KUZIFIKIA NDOTO ZAO

    June 20, 2024
  • Angalia Zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LA MADIWANI LA WILAYAYA ITILIMA LAUFUNGA MWAKA WA FEDHA WA 2020 - 2021
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Business License
  • Procedure for Provision of Buliding Permit
  • https://www.nbs.go.tz/index.php/en/census-surveys/population-and-housing-census/802-sensa-ya-watu-na-makazi-ya-mwaka-2022
  • Land Ownership

Tovuti Mashuhuri

  • Simiyu Regional Commissioner's Office
  • President's Official Website
  • Local Government Revenue Collections Dashboard
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Salary Slip Self Service
  • FFARS LINK
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    DED - ITILIMA

    Sanduku la Posta: 308 BARIADI

    Simu: +255 28 29 863 29

    Simu: 028 29 863 28

    Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa