Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Bi. Faraja P. Msigwa |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itilima Bi. Faraja P. Msigwa Awataka Watumishi kukubariana na mabadiriko yanayo tokea katika UTUMISHI wa umma.
Aliongea na Walimu wa Itilima katika ziara ya Kaimu Mkurugenzi wa Elimu Tamisemi, Bi. Faraja alisema.
"Kwa Sasa katika UTUMISHI wa Umma tuna Mfumo wa Upimaji wa Utendaji Kazi kwa Watumishi na Taasisi za Umma
(Pepmis na Pipmis) tuhakikishe tunajaza taarifa zote muhimu zinazo takiwa Kila Siku, ni jambo Muhimu sana kwa Serikali na kwa Mtumishi husika"
Kupitia Mfumo huu Serikali itabaini uwajibikaji na uhitaji wa rasilimali watu na kwa Mtumishi kuainisha majukumu ya utekelezaji ya Kila suku na kutoa fursa ya kupanda ngazi Mbalimbali za kiutumishi.
Aidha Bi. Msigwa akiwasilisha Shukrani za Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kushusha Fedha kwa Kiasi kikubwa katika Wilaya ya Itilima na kupelekea Mabadiriko makubwa katika Miundombinu ya Elimu kwa kipindi cha kifupi sana Cha Uongozi wake na kupelekea kuwa na Shule mpya nyingi za Msingi na Sekondari.
Vilevile Bi. Faraja alitumia fursa hiyo kuwakumbusha Watumishi wote wa Umma wa Itilima kuwa kuna Maisha baada ya UTUMISHI wa Umma kumalizika hivyo ni Muhimu kwa Mtumishi kuwa na Maandalizi Sasa kwa kujiwekea Hakiba au hata kuwekeza katika hisa kama za UTT, na kutumia muda VIZURI baada ya Muda wa Muajiri kujiimalisha kiuchumi
"JAMANI naongea haya naona baadhi ya Watumishi wenzetu waliomaliza muda wao jinsi wanavyo kabiliwa kabiliwa na ugumu wa Maisha, Kuna Maisha baada ya UTUMISHI wa UMMA tujipange"
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa