Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Kihongosi ameshiriki Zoezi kuwaapisha Wajumbe wa BARAZA la ardhi na Nyumba la Wilaya ya Itilima, ikiwa ni Rasmi kwa Baraza hilo kuanza kuhudumia Wananchi wa Wilaya ya Itilima.
Aidha wajumbe hao walioapishwa watakuwa na Jukumu la kuhudhuria Vikao vya Baraza na kusikiliza kesi na kutoa Maoni Yao kwa Maadhishi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Kihongosi akitoa Rai na kuwataka wajumbe wa Baraza la Ardhi kuwa waadilifu |
Aidha Mhe.alsema "Wajumbe Mnapaswa kuzingatia Miiko ya Wajumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya kama ilivoainishwa na Sheria ya Mahakama ya Ardhi Na 2 ya Mwaka 2002 na Kanuni ya 172 ya Mwaka 2003 na Mwongozo wa Sheria za Mahakama ya Ardhi ya Mwaka 2005"
Mhe. KIHONGOSI aliainisha Sheria hizo ambazo ni
1. Kuwa Mtu mwenye kujiheshimu
2. Kuishia na uonekane ni Mtu usiye na upendeleowa aina yoyote.
3. Usishiriki kutoa Maamuzi au Kusikiliza kesi yoyote itakavyo kuhusu wewe Binafsi au Mtu yoyote kutoka katika Familia Yako.
4. Ujue mipaka ya Kazi Yako na kwa namna yoyote usijaribu au kuonyesha kuwa wewe unafanya Kazi za Mwenyekiti.
5. Wakati wote uwe msiri kuhusiana na kesi ambazo bodo kutolewa uamuzi, hairusiwi kusema nje ya Baraza kitu chochote kinacho hisu undani wa kesi ambayo haija hamuliwa.
6. Haurusiwa kuwa na Urafiki wa Upande wowote na upande wowote katika kesi inayo endelea kusikilizwa
7. Hairusiwi kuwa wakili wa Upande wowote katika kesi, hairusiwi kutoa Ushauri au kuwaandikia wadaiwa kitu chochote katika kesi.
8. Kujiepusha na kuzungumza au kufanya Mawasiliano yoyote na wadaiwa katika eneo la Baraza na kwa Hali yoyote hairusiwi kutoka nje ya Jengo la Baraza kwenda kuzungumza na Wadaiwa au jamaa zake kabla au baada ya Saa za Kazi.
9. Kuwahi na kuhudhuria katika Vikao kama itakavyo kuwa imepangwa na Mwenyekiti na usikose kuhudhuria mfululizo wa Vikao kwa. Kipindi kisicho dhidi Mwezi Mmoja bila sababu ya kuridhisha.
10. Usimshawishi Mwenyekiti wa Baraza ili akupangie uketi kwenye kesi Fulani
11. Baada ya Kukamilika kusikilizwa kwa kesi Fulani mjumbe utatoa Maoni Yako kwa Maadhishi bila kuchelewa.
12. Usipokee au kuomba zawadi kama hongo na takrima kutoka upande wowote wa wadaiwa.
Wajumbe wa Baraza la Ardhi wakisaini HATI ya Kiapo baada baada ya Kila kiapo |
Mhe. KIHONGOSI alihitimisha kwa kuwatakiwa Wajumbe hao utekelezaji mwema wa majukumu Yao mapya kwa wanaitilima.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Anna Gidarya alisema
"Sasa tuna Imani kesi hizi za Ardhi zinaenda kupata utatuzi"
Aidha Mhe. Gidarya alimuomba Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kufikisha salamu za Wanaitilima kwa Mhe. RAIS, Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kutusogezea Huduma hii kwa Wananchi na Mimi kama Kiongozi wao naahidi tutalilea Baraza ili lihidumia Wananchi kwa Weledi, ili kuendelea kuunga Mkono Jitihada za Mhe. RAIS za kusogeza Huduma Muhimu kwa Wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Anna Gidarya akielezea Changamoto waliyo ipitia wanaitili huku wakisafiri kwenda kutafuta huduma ya Baraza Wilaya ya Maswa |
Awali, Kaimu Katibu Tawala ambaye ni Afisa Sheria wa MKOA wa Simiyu Bi. Mwanahamisi Kawega akiwasilisha Taarifa Kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa yakwambwa.
Tangu uanzishwe Mkoa wa Simiyu kumekuwa na Baraza la Ardhi na Nyumba katika Wilaya ya Maswa na limekua likihudumia Mkoa mzima wa Simiyu.
"Lakini kwa idhini ya Mhe. Rais. Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwaka Jana tulizindua Baraza kingine katika Wilaya ya Busega na Sasa tunawaapisha Wajumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Itilima lakini Mpango iliyopo ni Kila Wilaya ifikiwe na Huduma ya Mabaraza ya Ardhi.
Kwa upande wa Kamishna wa Ardhi Mkoa Alimshukuru Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa Kuwaapisha Wajumbe wa Baraza la Ardhi la Itilima, na Kuushukuru Uongozi wa Wilaya ya Itilima Kwa kulipatia Baraza Jengo litakalo tumika kama Ofisi ya kutekeleza Majukumu ya Mbalimbali ya Baraza.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa