• MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
Itilima District Council
Itilima District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Sisi ni nani?
    • Dira na Dhamira
    • Taarifa ya Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango
      • Afya
      • Mifugo
      • Kilimo
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi
      • Sheria
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
    • Muundo
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Ujenzi
    • Leseni za Biashara
    • Umilikaji wa Ardhi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba Video
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi inayofadhiliwa na Wahisani
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea na Ujenzi
    • Maandiko ya Miradi
  • Zabuni
  • Uwekezaji
  • FFARS LINK

Waziri Mkuu Majaliwa Mgeni Rasmi Maonesho ya SIDO Kitaifa Simiyu

Posted on: October 9th, 2018

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maonesho ya Kwanza ya Viwanda vidogo (SIDO)  ambayo Kitaifa yatafanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka  katika kikao cha maandalizi ya maonesho  hayo kilichowashirikisha baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na mameneja wa Shirika la Viwanda vidogo (SIDO) kutoka mikoa ya Simiyu, Dodoma ,Mwanza, Kagera ,Mara, Shinyanga na Arusha.

Mtaka amewakaribisha wananchi wa mkoa mwenyeji Simiyu Watanzania wote kwa ujumla kuja kushiriki maonesho ya SIDO yatakayobebwa  na Kauli Mbiu “Pamoja Tujenge Viwanda Kufikia Uchumi wa Kati” na kubainisha kuwa mkoa wa Simiyu unaamini kuwa maonesho hayo yatakuwa ni maonesho darasa, mahali ambapo watu watajifunza na kufanya biashara.

Ameongeza kuwa maonesho ya SIDO yanabeba ajenda ya Serikali ya awamu ya tano na matamanio ya Mhe. Rais ya kuwa na Tanzania ya Viwanda na kuifikisha  nchi katika Uchumi wa Kati, hivyo akaawaalika wadau wote wenye teknolojia mbalimbali kushiriki maonesho haya.

“Ninawaalika wadau wote wenye teknolojia mbalimbali waweze kushiriki maonesho haya , nayaalika makampuni, taasisi na mashirika yenye vitu vinavyoweza kuwafaa wajasiriamali na Watanzania ambao wangehitaji kuwekeza kwenye viwanda, waweze kuleta teknolojia zao”

“Ninawaaalika Wajasiriamali wote kushiriki maonesho haya maana yatatoa nafasi kila mjasiriamali kujifunza kwa mwenzake, kupata elimu na kubadilisha ujuzi ili waweze kuzalisha bidhaa bora zaidi” alisema Mtaka

Aidha, ametumia mkutano huo kuzialika taasisi za fedha ili ziweze kujitangaza kwa wajasiriamali nao wakaona ni namna gani wanaweza kupata mitaji, huku akisisitiza na kuzialika taasisi za kitaaluma na vitivo vya uhandisivya Vyuo vikuu  pamoja na mashirika mbalimbali ya Kimatifa yanayofanya kazi hapa nchini.

Akizungumzia ada ya ushiriki Mtaka amesema wajasiriamali wenye mahitaji maalum watashiriki bure, wajasiriamali wadogo watashiriki bila kulipia gharama yoyote isipokuwa watalipa shilingi elfu kumi (10,000/=)  kwa ajili ya sare, wajasiriamali wa kati watachangia shilingi laki mbili (200,000/=) taasisi, makampuni na mashirika ambayo hayapo katika makundi la wajasiriamali wadogo , wa kati na wadhamni watatakiwa kuchangia shilingi milioni mbili (2000,000/=) kama ada ya ushiriki.

Kwa upande wa udhamini Mtaka amesema kuwa kwa taasisi, mashirika au kampuni zilizo tayari kudhamini maonesho hayo,  kiwango cha juu kitakuwa shilingi milioni thelethini (30,000,000/=), kiwango cha kati shilingi milioni kumi  (10,000,000/= ) na kiwango cha chini kitakuwa milioni tano (5,000,000/=)  huku akisisitiza kuwa  wadhamini hawa watambuliwa kwa vyeti na watapewa kipaumbele cha mgeni rasmi kutembelea mabanda yao.

Jumla ya  wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa 1000 wanatarajia kushiriki Maonesho haya ya Viwanda Vidogo SIDO Kitaifa pamoja na taasisi, mashirika na makampuni ya Umma na binafsi yatashiriki pia

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA WILAYANI ITILIMA October 30, 2021
  • Tangazo Kwa Watumishi Wapya Wanao endelea kuwasili Wilayani Itilima July 03, 2022
  • "Tutaukaribisha Mwenge wa Uhuru Wilayani Itilima tarehe 9/7/2022 tutaupokea katika Viwanja vya Ushirika, Nyamalapa na mkesha utakuwa katika viwanja vya Halmashuri ya Wilaya ya Itilima Wananchi wote, Wafanyakazi tuungane katika makaribis July 07, 2022
  • "Tutaukaribisha Mwenge wa Uhuru Wilayani Itilima tarehe 9/7/2022 tutaupokea katika Viwanja vya Ushirika, Nyamalapa na mkesha utakuwa katika viwanja vya Halmashuri ya Wilaya ya Itilima Wananchi wote, tuungane katika kuukaribisha Mwenge July 06, 2022
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • TUME YA TAIFA YA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI YAPIMA NA KUKABIZI HATI ZA VIJIJI 25 VILIVYOPO KANDO YA POLI LA AKIBA LA MASWA

    June 30, 2024
  • BARAZA LA ARDHI ITILIMA SASA RASMI BAADA YA KUAPISHWA KWA WAJUMBE WA BARAZA

    June 26, 2024
  • KUNA MAISHA BAADA YA UTUMISHI WA UMMA

    June 20, 2024
  • MWALIMU TIMIZA WAJIBU WAKO WA MSINGI KWA AJILI YA NCHI YAKO, WAZAZI WA TANZANIA NA WATOTO KUZIFIKIA NDOTO ZAO

    June 20, 2024
  • Angalia Zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LA MADIWANI LA WILAYAYA ITILIMA LAUFUNGA MWAKA WA FEDHA WA 2020 - 2021
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Business License
  • Procedure for Provision of Buliding Permit
  • https://www.nbs.go.tz/index.php/en/census-surveys/population-and-housing-census/802-sensa-ya-watu-na-makazi-ya-mwaka-2022
  • Land Ownership

Tovuti Mashuhuri

  • Simiyu Regional Commissioner's Office
  • President's Official Website
  • Local Government Revenue Collections Dashboard
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Salary Slip Self Service
  • FFARS LINK
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    DED - ITILIMA

    Sanduku la Posta: 308 BARIADI

    Simu: +255 28 29 863 29

    Simu: 028 29 863 28

    Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa