Na. Haruna Taratibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki Aahidi ujenzi wa Maabara na Nyumba mbili za Walimu wilayani Itilima.
Akiwa katika ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Elimu Wilayani Itilima Mhe. Kairuki alisema"Tamisemi itaendelea kuboresha Miundombinu ya Elimu ikiwemo ujenzi wa Maabara katika Shule za Sekondiari na katika kipindi hiki watajenga Nyumba mbili za Walimu"
Aidha akijibu Ombi la Diwani wa Kata ya Bumera Mhe. Mboje Mhuli la Kuomba kujengewa Maabara na Bweni Mhe. Kairuki alisema ya Kwamba suala la Maabara Serikali italifanyia kazi ombi Hilo kuhusiana na Bweni alishauli uwepo uhamasishaji wa wananchi kujenga Hosteli iliwa wanafunzi wanao Kaa mbali na shule waezekupata huduma ya kuishi karibu na Shule.
Mhe. Kairuki alikagua mradi wa chumba kimoja cha darasa katika shule ya Sekondari ya Madilana, vyumba vitano vya katika shule ya Sekondari ya Kanadi, vyumba viwili vya Madarasa katika shule ya Sekondari Ikindilo na vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Sekondari Habiya.
Katika ziara hiyo Mhe. Mhe. Kairuki aliridhishwa na utekelezaji wa miradi unavyo endelea Wilayani Itilima na kiwataka wahandisi wa Itilima kufuata maelekezo yote yaliyo tolewa na Mhandisi wa Mkoa Mhandisi Mashaka Luhamba aliye shauri uongezaji wa vyuma katika Madirisha Kwa ajili ya usalama wa Mali zilizopo ndani ya darasa.
Utekelezaji mradi wa ujenzi wa vyumba vya Madarasa upo katika hatua ya umaliziaji ambapo Itilima inatekeleza mradi wa ujenzi wa vyumba 27 vya Madarasa katika shule za sekondari 16 baada ya Itilima kupokea kiasi cha Tsh. Milioni 540/= kutoka serikali kuu
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa