Uongozi wa Wilaya ya Itilima umewaonya baadhi ya watu wanahujumu miundombinu ya maji iliyojengwa na wadau wa maendeleo Wilayani humo kwa ajili ya kusogeza huduma hiyo muhimu kwa jamii.
Aidha imebainika kuwa licha ya wadau wa maendeleo wilayani humo kujitahidi kutumia gharama kubwa ili kuwasogezea wananchi huduma muhimu kwa lengo la kuwasaidia kuondokana na adha mbalimbali zinazowakabili baadhi ya watu wamekosa uaminifu na kuamua kufanya uharibifu.
Onyo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Faidha Salim wakati akikagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Shirika lisilo la Serikali la World Vision na kusema kuwa Mamlaka haitosita kuchukua hatua dhidi ya watu/mtu yeyote atakayebainika kufanya uharibifu kwenye mradi wowote wa maendeleo.
Mhe. Faidha amesema kuwa kufanya hivyo ni kuwakatisha tamaa wadau waliojitoa kwa ajili ya maendeleo na kusaidia wananchi kuondokana na changamoto zinazowakabili, alisisitiza kuwa hatamvumilia yeyote atakaye patikana kuhujumu miradi.
Ameongeza kuwa kila mmoja anao wajibu wa kulinda na kuitunza miradi ili isiharibiwe kwa ajili ya manufaa ya kizazi hiki na kijacho huku akikisitiza utoaji taarifa dhidi ya inayoharibiwa kwa ajili ya manufaa ya vizazi vyao na vijavyo.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Kilugala Lulu Mang'ombe ameeleza kuwa kabla ya kupata mradi huo walikuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu wa Kilomita 5 kwenda kutafuta maji ambapo yalikuwa ya kwa shida.
Akieleza juu ya uharibifu wa mradi wa maji Mang'ombe amekiri kufanyika kwa uhujumu katika mradi na hii ni kutokona na kusitishwa kuchota maji bure na kulazimika kulipia jambo lililopelekea sintofahamu kwao na kusababisha tatizo hilo na hii ni kwa sababu ya ukosefu wa elimu ya kutosha juu ya mradi huo ambapo kwa sasa imeanza kutolewa.
Kwa upande wa Mratibu wa mradi wa Kanadi na Luguru Nyamoko amesema kuwa mradi huo wa Kilugala umegharimu kiasi cha Tshs. Milioni 460/ na unauwezo wakuhudumia wakazi zaidi ya 8, 000 pamoja na vijiji 3.
Aidha Mratibu huyo aliainisha Miradi mingine iliyofadhiliwa na Shirika hilo ni pamoja na ujenzi wa vyoo matundu 8 katika shule ya Msingi Chinamili uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 42 ambapo wanafunzi zaidi ya 1000 wananufaika na mradi huo.
Ujenzi wa Zahanati ya Ikungulipu iliyopo katika kata ya Luguru umegharimu kiasi cha shilingi milioni 142 na unahudumia wagonjwa 80 kwa siku.
World Vision inatekelezaji wa Mradi wa Maji katika Kijiji cha Nangale kilichopo katika Kata ya Ndoleleji Mradi huo Unajumuisha Tenki lenye ujazo wa Lita elfu 50, na vituo vya kuchotea maji vitano na nyumba ya Mitambo kwa ujumla mradi umegharimu kiasi Cha Tshs. Milioni 217/- na utahudumia wakazi zaidi 2000.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa