Na. harunataratibu82@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Faidha S. Salim ameishukuru TANAPA Kwa kuvipatia Mizinga 171 ya Nyuki navifaa vya kulinia Asali Vijiji 9 vinavyo pakana na Poli la Akiba la Maswa Mhe. Faidha alisema
" Kupata miradi ya Nyuki kama hii na miradi mingine isiyo husisha kilimo au kuathiriwa na wanyama wakali tutakua tumeiokoa jamii, hata sisi viongozi tutakuwa na chakusema jamani hatujafanikiwa kwenye kilimo lakini kuwawezesha kupata kipato Kwa njia nyingine tumefanikiwa"
Aidha Mhe. Faidha aliomba ushirikiano huu uendelee na kuendelee kutoa mizinga zaidi kwani vijiji hivyo 9 vina Wananchi wengi zaidi.
Kwa upande wa Mratibu wa Mradi Kutoka TANAPA Ndg. Daniel alisema Mradi huu ni matokeo ya Ushirikiano wa Tanzania na Ujerumani katika utunzaji Bainuai katika mazingira na katika ushirikiano huo ndio ukaleta mradi huu katika wilaya Tatu za Itilima, Meatu na Maswa na ulianza Novemba 2022.
Aidha Mratibu huyo wa Tanapa alisema Mradi huo unatekelezwa katika vikundi 16 katika wilaya zote tatu Kwa Itilima unatekelezwa katika vikundi 9.
Wilaya ya Itilima imepokea Mizinga 171 yenye thamani ya Sh. Milioni 54 kati ya Mizinga 300 iliyotolewa Kwa wilaya zote tatu ikiwa na thamani ya Sh. Milioni 94/
Sanjari na ugawaji wa Mizinga hiyo Tanapa wataendesha mafunzo maalumu ya matumizi ya Mizinga hiyo kuhakikisha vikundi vyote vinatekeleza mradi hua Kwa tija.
Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe. Njalu D. Silanga aliwapongeza Tanapa Kwa kutoa kipaumbele cha pekee kwa wanaitilima kupata mizinga 171 Kwa vikundi tisa na huu ni uchumi watu watafanya, a biashara ya Asali alisema Mhe. Njalu.
Aidha Mhe. Njalu aliwaasa wanavikundi kwenda kuyasimamia Yale yote watakayo elekezwa Kwa lengo la kiuchumi na usalama dhidi ya wanyama hatari na waharibifu kama Tembo.
Akiwakilisha Vijiji 9 vinavyo tekeleza Mradi huo, Diwani wa Kata ya Nkuyu Mhe. Ndulu Buyenze Ntegwa alisema
" Miaka mingi nyuma tumekua hatuoni mambo kama haya na tumekua tukisikia kwamba sisi wananchi wa vijiji vya kandokando mwa Poli @njalusila
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa