|
Na. harunataratibu82@gmail.com
Halmashauri ya wilaya ya Itilima nimiongoni mwa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu zilizo kusanya mapato kwa zaidi ya asilimia 100 .
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri katika kikao Cha Baraza la Madiwani katika kipindi Cha julai 2021 hadi tarehe 30 Juni 2022 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itilima Bi. Elizabeth Gumbo alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itilima Bi. Elizabeth Gumbo |
Halmashauri ya Wilaya ya Itilima ilikisia
Kukusanya jumla ya Tshs. Bilioni 1.48 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani Kwa mwaka 2021 - 2022, mpaka Juni 2022 Halmashauri ilikusanya jumla ya Tshs. 1.577. ambayo ni sawa na asilimia 106 ya makisio ya mapato.
Kufuatia taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji kuhusiana na Ukusanyaji wa mapato na taarifa iliyosomwa na Waziri wa Nchi katika ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Innocent Bashungwa kuwa makusanyo ya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima kwa mwaka wa fedha 2021 - 2022 ni asilimia 91 kutoka kwenye makasio ya Tsh. Bilioni 1.48.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Faidha S. Salim amemuagiza Mkurugenzi wa Mtendaji kuandika barua kupitia Kwa katibu tawala wa Mkoa Kwenda Tamisemi Kwa lengo la kuweka takwimu sahihi.
"Tulistahili makusanyo yetu yasomeke asilimia 106 na sio asilimia 91" alisema Mhe. Faidha.
Aidha katika kikao hicho Cha Baraza kilitekeleza maazimio yaliyo wekwa katika kikao kilichopita kuhusu kutoa motisha kwa kata zitakazofanya vizuri katika Makusanyo ya Mapato.
Kata ya Lagangabilili iliibuka kinara kwa kukusanya kiasi Cha shs. Milioni 21, na Mtendaji kupewa motisha ya Shs. 100,000/ nje ya asilimia Tano ya makusanyo ambayo mkusanyaji hupatiwa.
Kata ya Mwaswale ilishika nafasi ya pili, ikifuatiwa na Kata ya Migato ilishika na fasi ya tatu , Budalabujiga nafasi ya nne na nafasi ya Tano ilishikiwa na kata ya Mwamapalala.
Aidha kuhusiana na suala Zima la makusanyo kuwa ajenda muhimu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Mhe. Saudi Nyalamo aliwaasa Madiwani na Watendaji wa Kata kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa Mapato ili kuiweka Halmashari katika nafasi nzuri.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itilima Mhe. Daud Nyalamo |
Akiongea Kwa niaba ya watendaji waliopata motisha baada ya kufanyavizuri Phabiani Phabian ambaye anaiwakilisha Kata kinara ya Lagangabilili alisema
" Kitendo cha uongozi kutoa motisha kwa wanao fanya vizuri katika makusanyo ni Jambo jema ambalo litaleta ushindani haliyakua halmashauri yetu ikipata takwimu nzuri za makusango"
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa