Mpango wa kunusuru kaya masikini unao ratibiwa na Tasaf, ukiwa katika Miaka mitano ya Utekelezaji na miaka minne ya malipo umekuja na Mradi mwingine wa kuwajengea uwezo kiuchumi wanufaika wa Mpango huo kwa kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa.
Mradi huo ambao unaanza na Halmashauri 44 kati ya 186 nchini, Itilima ikiwemo, umetoa mafunzo ya kuweka na kukopa fedha kwa wanufaika wote wa Tasaf ili kuwajengea uwezo wa kuendesha vikundi vyao.
Akizungumza na Wananchi wa Kata Zagayu na Kinang’weli ofisa wa Tasaf kutoka Kitengo cha kuweka akiba na kukuza uchumi wa Kaya Bi. Anzanukye Mselela alisema
“ Mkiwa kwenye vikundi na mkajiwekea akiba, pesa ya Tasaf ikichelewa, pesa za kwenye kikundi ziwasaidia kwa kukopeshana wenyewe kwenye vikundi na kutozana riba yenye tija kwa lengo la kuimarisha kikundi ili kiendelee kuwahudumia”
Aidha Bi. Mselela alisema “ili vikundi viwe na tija vitasajiliwa Serikalini na mkiweza kama kikundi kuwa na mradi mwingine itakuwa vyema zaidi na kitaweza hata kushiriki kwenye maonyesho mbalimbali ya Kitaifa kwa kusafirishwa na serikali”
Mratibu wa Tasaf wilaya ya Itilima ambaye ni Mtaalam wa Maendeleo ya Jamii Ndg. John Rajabu aliwaasa wanufaika hao wa Tasaf kuto dharau vikundi hivyo kwani vikipata usajili vitaweza hata kushirikishwa katika miradi mingine na hata kunufaika na asilimia 10 ya kisheria inayo tolewa na Halmashauri kwenye Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.
Sanjari na hayo, Mlezi wa Tasaf wilaya ya Itilima Paulo Tibahilila aliwataka wananchi wa Kata hizo kuhakikisha wanapata Vitambulisho vyao vya taifa au namba ya kitambulisho ilikuweza kusajili Simu zao kwa alama za vidole ili kuepuka usumbufu kwa siku zijazo.
Vilevile Tibahilila aliwataka wanufaika hao kutoa taarifa wanapo pata watoto na familia kuongezeka ili taarifa ziweze kubadirishwa kwenye mfumo ili kuepuka kupunjwa stahili zao.
Mpango huu wa kunusuru Kaya masikini unao ratibiwa na Tasaf ukiwa katika miaka mitano ya utekelezaji na minne ya Malipo umefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuwawezesha na kuwatoa wananchi walengwa kenye hali duni iliyo kithiri na sasa unawapeleka katika hatua nyingine ya kuwajengea uwezo kupitia vikundi vya kuweka na kukopa
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa