Naibu waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anaye shughulikia Watu wenye Ulemavu Stella Ikupa amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka kwa jitihada zake za Makusudi za kunyanyua Maendeleo ya Mkoa wa Simiyu hususani katika sekta ya Elimu.
Akizungumza katika kilele cha ufungaji wa Makambi maalimu ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne Mhe. Ikupa alisema
"Nampongeza Mkuu wa Mkoa kwa ubunifu huu wa kuandaa Makambi haya naamini wanafunzi mmejifunza mambo mengi na mtafanya vizuri katika mtihani wenu na ningeshauri viongozi wengine waige jambo hili"
Aidha Mhe. Ikupa alisema serikali inaendelea kuboresha sekta ya Elimu nchini kwa kuongeza bajeti katika Shule, kujenga madarasa na itaendelea kutatua changamoto za Walimu katika Mkoa huu na Nchi kwa ujumla.
Akiongea na hadhara hiyo Mhe. Mtaka alisema
" kwa uwekezaji uliyofanyika kwa watoto hawa na walimu mahili kwa kushirikiana na viongozi wazazi na wadau mbalimbali naamini watafanya vizuri Mitihani yao ambayo itaanza hapo Novemba 4, mwaka huu"
Aidha Mhe. Mtaka alisema Kama Mkoa wataendelea kutoa motisha kwa Walimu na watoto watakao Fanya vizuri katika matokeo ya kitaifa.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abas alisema kuwa kupitia Kambi hii anamatumaini ya kuwa kutapatikana Viongozi mahiri na kuahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za wanafunzi kutimiza ndoto zao.
Kwa niaba ya Chama cha Walimu Tanzania CWT katibu Mkuu wa chama hicho Ndg. Deus Seif aliunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa katika maendeleo ya Elimu kwa kutoa Mifuko 500 ya Saruji na kuwashukuru Walimu kwa kujitoa kwao na ushirikiano waliyo uonyesha.
Akitoa maelezo ya kina kuhusiana na Kambi hii Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu Ndg. Elnest Hinju alisema
" Kambi ilikuwa na jumla ya wanafunzi 1512 ambao walipata fursa ya kukaa kambini kwa takribani miezi miwili na kufundishwa na walimu mahili, kusoma kwa bidii pamoja na kujifuza masuala mbali mbali ya kijamii"
Akiwakilisha wanafunzi waliyo hudhuria katika Kambi hiyo Mwanafunzi Magreth Sonda kutoka shule ya sekondari Simiyu alisema
"Kupitia Kambi hii tumejifunza mambo mengi kwa Walimu wetu ikiwemo mbinu mbali mbali za ujibuji wa maswali na kwa mitihani tuliyofanya ufaulu wetu umekuwa ukipanda na naamini tutafanya vizuri mitihani yetu ya mwisho.
Tangu Kambi hii zianze rasmi mwaka 2016 zimesaidia kuongeza kiwango cha ufaulu katika matokeo ya kidato cha nne ambapo mwaka 2017 ufaulu ulikuwa 70.68% na mwaka 2018 ufaulu ulikuwa 86.46% na Simiyu kushika nafasi ya 9 kitaifa.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa