Na. Haruna Taratibu
Serikali ya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya imeitengea Itilima kupitia TARURA kiasi cha Tshs. Milioni Bilioni 2.37 Kwa ajili ya matengenezo ya KM. 238.88 za Barabara.
Fedha hiyo itahusisha ujenzi wa madaraja makubwa matatu na madogo 8, Makaravati 31, ujenzi wa Mitaro na ujenzi wa Km. Moja Kwa kiwango cha Lami makao makuu ya Wilaya ya Itilima.
Ujenzi wa km. 1 ya Lami umetengea kiasi cha Tshs. Milioni 500/ kutoka Mfuko wa Barabara na ujenzi utaanzia pale Mradi wa Lami wa awali ulipoishia na kuelekea Barabara ya Mzunguko (Roundabout) ya kuelekea Hospitali ya Wilaya.
Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi Kampuni ya M/S CIVMARK LIMITED ya ya Dar Es Salaam kwa Gharama ya Tshs Milioni 499.89 Kwa kipindi cha Miezi 6.
Wilaya ya Itilima katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uo ngozi wa Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Bajeti ya barabara imeongezeka Kwa zaidi ya mara nne.
Kuongezeka huko Kwa bajeti kumepelekea Itilima kuwa na Km. 248.34 za barabara nzuri, km. 164.21 za barabara za wastani na Barbara zisizopitika no Km. 123.16 sawa na asilimia 23.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa