Na. Haruna Taratibu
Halmashauri ya wilaya ya Itilima ni Miongoni mwa Halmashauri zilizo kidhi vigezo vya kupewa fedha za awamu ya Pili kutoka Mfuko was Maendeleo Tasaf Kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Katika Fedha hizo kiasi cha Tshs. Milioni 92.4/= zinaenda kutekeleza Mradi wa Jengo la Utawala Katika Shule Mpya ya Sekondari ya Nguno, na TShs. Milioni 70.6/= inaenda kujenga Vyumba viwili vya Madarasa na Matundu SITA ya vyoo katika shule hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Bi. Elizabeth Gumbo akikagua Mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Inalo inayo tekelezwa na fedha za Tasaf wakati ukiwa katika hatua za awala |
Aidha Miradi Mingine itakayo tekelezwa ni pamoja na ujenzi wa Vyumba viwili vya Madarasa katika shule ya Msingi Mwazimbi pamoja Matundu SITA ya Vyoo baada ya kupokea fedha kiasi cha Tshs. Milioni 68.3.
Mradi wa Bweni la wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Shishani unao tekelezwa Kwa fedha kutoka Tasaf ukiwa umekamilika kwa hatua ya awali, kuelekea hatua ya ukamilishaji.
Shule ya Msingi Mwabasabi iliyopo katika Kata ya Budalabujiga imepata fedha kiasi cha Tshs. Milioni 68.3 kuanza Mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa na matundu SITA ya vyoo.
Sanjari na hayo Mradi wa Ujenzi wa Bweni katika shule ya Sekondari Shishani umepokea tena fedha kiasi cha Tshs. Milioni 76.6 Kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Bweni hilo lenye uwezi wa kuhudumia wanafunzi 80.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango wakikagua Mradi wa Bweni katika shule ya sekondari Shishani, mradi unatekelezwa na fedha kutoka Tasaf |
Katika awamu ya kwanza Wilaya ya Itilima ilipokea fedha kiasi cha Tshs. Milioni 451/= na kutekeleza Mradi wa Vyumba viwika vya Madarasa na Matundu SITA ya vyoo shule ya mpya ya sekondari Nguno.
Aidha fedha hizo za awali zinaendelea kutekeleza Mradi wa ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Gambasingu, Inalo na Mwagimagi ambapo ujenzi upo katika hatua za umaliziaji na Ujenzi wa Bweni katika shule ya sekondari Shishani.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa