Haruna Taratibu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeridhishwa na utekelezeji Mradi wa Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Nhobora iliyopo katika Kata ya Nhobora wilayani Itilima na kuipatia rasmi Shule hiyo usajili mnamo tarehe 8/11/ 2022 na itaanza rasmi kupokea wanafunzi Januari 2023.
Aidha, Shule hiyo iliyojengwa baada ya Halmashauri ya Itilima kupoke fedha za Mpango wa uboreshaji Elimu Kwa shule za Sekondari (SEQUIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kiasi cha Tshs. Milioni 470/- kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba nane vya Madarasa, Vyumba vitatu vya Maabara , Jengo la Utawala, chumba cha Kompyuta, jengo la Maktaba na matundu 10 ya vyoo vya Wavulana na 10 vya Wasichana.
Shule hiyo itakayo milikiwa na Wananchi wa Wilaya ya Itilima kwa kushirikiana na Mkoa itakuwa ya Kutwa, Mchanganyiko na yenye mikondo miwili na namba yake ya Usajili ni S.5952.
Jamii ya Wanaitilima hususani wakazi wa Kata ya Nhobora wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuzielekeza fedha hizi katika Kata ya Nhobora ambayo haikuwa na Shule ya Sekondari, Iliwalazimu wakazi wa Kata hiyo kuwapeleka watoto wao katika Kata Jirani za Luguru na Mbita Kupata Elimu ya Sekondari.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa