MKUU wa mkoa wa Simiyu,David Kafulila amepiga marufuku kwa magari madogo ya abiria yanafanya biashara ya kusafirisha watu maarufu kwa jina la Michomoko katika mkoa huo kuacha mara moja kwani wanakiuka masharti ya leseni zao.
Pia magari hayo yamekuwa ndiyo chanzo cha ajali katika mkoa huo na kusababisha kupoteza maisha ya watu na kuwapatia vilema vya maisha.
Rc Kafulila amefikia Uamuzi huo kufuatia ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo ya Magereza nje kidogo ya mji wa Bariadi ambapo watu watano waliopoteza maisha na wengine kumi na moja kujeruhiwa.
Kafulila ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo ambapo alisema vyombo hivyo vya usafiri pamoja na wamiliki wake wamekuwa hawafuati maelekezo ya serikali ikiwemo mamlaka ya udhibiti usafirishaji wa ardini (LATRA).
Amesema pamoja na hatua zingine za kiutawala zinazoendelea kutokana na ajali hizo yeye kama mkuu wa Mkoa aamua kufanya maamuzi ya kimfumo kwa maana ya kwamba hizo gari zinasajiliwa kwa ajili ya kufanya kazi na zinafanya kama daladala (tax).
Amesema inafahamika kwamba Ili gari zifanye kazi kama daladala, kuna utaratibu wake ikiwemo rangi na alama pamoja na namba ili kusudi likitokea tatizo lolote lile iwe rahisi kufahamika na kuziratibu.
"Wamiliki na waendeshaji wa michomoko kwa zaidi ya nusu mwaka wameshapewa maelekezo ya taratibu za kufuatia Ili kusudi waendelee na kazi hizo za usafirishaji lakini mpaka Sasa hakuna gari iliyotekele hayo maelekezo Ili isajiliwe" amesema Kafulila.
Amesema kuwa kutokana na ajali hizo zimekuwa zikighalimu maisha ya watu, kusababisha ulemavu na kutokana na ukubwa wa jambo lenyewe nimeelekeza kuanzia leo gari zote aina ya michomoko hazipaswi kuonekana barabarani zikifanya biashara ya usafirishaji wa abiria mpaka itapo amliwa vinginevyo.
Aidha ametoa wito kwa wamiliki wa magari ya abiria na wawekezaji katika sekta ya usafirishaji wake katika soko la Simiyu kwa huo ni usafiri salama zaidi na kunauhitaji mkubwa wa magari ya abria Ili kuziba ukosefu wa usafiri.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa