Haruna Taratibu
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi - Afya Mhe. Dkt. Festo Dugange aridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Afya wilayani Itilima.
Mhe. Dugange alifanya ziara ya ukaguzi wa Mradi wa ujenzi Kituo kipya cha Afya cha Mwanhunda kilinajengwa katika kata ya Migato kwa fedha za Tozo kutoka serikalini kiasi cha Tshs. Milioni 500/
Akiwa kituoni hapo Mhe. Dugange aliuagiza uongozi wa Mkoa na Wilaya kuhakikisha kituo hicho kinanza kutoa tarehe huduma kwa wateja wa huduma za Nje kuanzia tarehe 1/2/2023 .
Aidha Dkt. Dugange alitoa wito Kwa uongozi Halmashauri kuhakikishaasilimia chache zilizo baki za ukamilishaji na utaratibu wa kujenga Nyumba ya Watumishi unaanza mapema.
Sanjari na hayo Dkt. Festo Dugange aliziagiza Halimashauri zote nchini kuhakikisha nyumba za watumishi zilizo jengwa katika hospitali zote za wilaya zinaanza kutumika Ili huduma Kwa wateja zitolewe kwa ufanisi zaidi.
Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Bi. Elizabeth Gumbo aliushukuru uongozi wa serikali ya Awamu ya SITA chini ya uongozi mahili wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha ujenzi wa kituo hiki cha Afya na alitoa Rai Kwa wananchi wa Migato
"Tuhakikishe tunailinda na kuitunza Miundombinu hii Ili iweze kuhudumia wananchi na kufikiwa kwa malengo yaliyo kusudiwa ya kuokoa maisha kwa kitoa huduma za dharula Kwa wakati.
Diwani wa kata Mhe. Ntobi Mbuga aliimshukuru Mhe. Rais Dkt. Simia Suluhu Hassan Kwa kuipatia Kata ya Migato kituo cha Afya, Kwa kipindi kirefu wakazi wa migato wamekua wakisafiri umbali mrefu kutafuta huduma za afya, uwepo kituo hiki utatatua changamoto zilizo kiwa zinawakabili wanamigato hususana Kwa wakina Mama wajawazito na watoto.
Mhe. Dkt. Dugange alikamilisha ziara yake kwa kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Itilima na aliipongeza kwa kuanza kutoa huduma za upasuani na huduma kwa Wateja wa Nje, Dkt. Dugange alisema
"Mpaka Sasa Serikali imeshaleta fedha hapa zaidi ya Bilioni 3/ na majengo 17 yamejengwa hapa na baadhi ya majengo yameanza kutoa huduma, niwa hakikishie serikali italeta vifaa zaidi n suala la wataalamu wa Mionzi serikali italifanyia kazi"
Wananchi wa Itilima kwa kipindi kirefu wamekuwa wakilazimika kusafiri katika wilaya ya jirani ya Bariadi na hata Mwanza Kwa ajili ya kufuata huduma za dharura, hali hii imekua ikisababisha baadhi Wakinamama wajawazito kupoteza maisha wakiwa njiani, hivyo basi uwekezaji huu wa serikali ya Awamu ya sita utatatua kwa kiasi kikuba changamoto hizo.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa