Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kutoka Tamisemi Ndg. Vicent Kayombo akiwasilisha maelekezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Tamisemi kwa Viongozi wanao Simamia Sekta ya Elimu Itilima na na kwa walimu wote Wa Itilima |
"Mwalimu ukitimiza Wajibu wako na Mwanafunzi akafaulu, Mzazi hufurahi na kukupongeza na kuipongeza Serikali na hata Mtoto anapopata matokeo mabaya Mzazi hulaani na kuchukia Serikali"
Hiyo nikauli iliyotokewa Ndg. Vincent Kayombo akimuwakilisha Mkurugenzi wa Elimu Tamisemi katika ziara ya kuongea na Walimu wa Itilima.
Walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakifuatilia Hotuba ya Kaimu Mkurugenzi wa Elimu Tamisemi, haionekani katika Picha. |
Ndg. Kayombo. Alisema yakuwa Serikali imeamua kwa dhati kushughurikia Changamoto zote za Walimu ikiwemo Madalaja, Malimbikizo na madeni ya likizo na Walimu wameanza kulipwa kwa awamu.
Aidha mwakilishi huyo wa Mkurugenzi wa Elimu Tamisemi aliwataka Walimu nao kutimiza majukumu Yao ya Ulezi wa Watoto kimaadili na Kitaaluma.
Haiingii akilini Mwalimu uliye ajiliwa na Serikali kwa Taaluma Yako uliyo isomea, inakuaje watoto unao wafundisha wanapata UFAULU wa 0 na kusababisha Wazazi kuichumia Serikali? Hali yakuwa unapata Mshahara Kila Mwisho wa Mwezi, jamani hii siyo haki alisisitiza Mwl. Kayombo.
Maafisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima waksikiliza kwa makini maelekezo ya Mkurugenzi wa Elimu Tamisemi |
JAMANI tujitafakari na tuanze upya kutimiza jukumu hili mlioaminiwa nalo na Serikali la kutengeneza vijana wa Tanzania ili nao kwa maarifa mliyo wapatia waje kuijenga nchi yao.
Sanjali na hayo Ndg.Kayombo alitoa maelekezo ya Mkurugenzi wa Elimu Tamisemi
Ambayo yaliwataka Walimu wakuu na wakuu wa Shule kuhakikisha Walimu nao wanapata chakula cha Mchana Shuleni ili aweze kutimiza majukumu Yao ya Siku kwa ukamilifu.
Maafisa Elimu wa Kata za Halmashauri ya Itilima wakifuatilia Hotuba ya Kaimu Mkurugenzi wa Elimu Kutoka Tamisemi, hayupo katika Picha. |
Pia, Maafisa Elimu wa Kata wameagizwa kutekeleza mabaraza ya Shule Watoto watoe maoni yao ikiwa pamoja na kuainisha unyanyasaji wote unaofanyika Shuleni.
Vilevile watoto waandaliwe Mazingira ili wachague wenyewe Mwalimu Mnasihi ili watoto wawe huru kuwasilisha Changamoto zao Kwa Mwalimu husika.
Afisa ELIMU Mkoa wa Simiyu Ndg. Khalifa Shemahonge aliongea na Walimu wa Itilima na kuwaasa kutimiza Wajibu wao wa kimalezi na Taaluma kwa Watoto ili tija ionekane |
Kwa upande wa Afisa ELIMU Mkoa wa Simiyu Ndg. Khalifa Shemahonge Alisema
"Tumetubu na tunaanza upya na ikumbukwe Kazi ya Utoaji wa Elimu ni Kazi ambayo Mwenyezi Mungu aliikasimisha kwa Mitume na Ndiyo maana Yesu alikuwa na Wanafunzi wake na Mtume Muhammad alikuwa na Maswahaba wake.Na Wanafunzi wote hawa baada ya kuelimika ndiyo walitekeleza malengo ya Mwenyezi Mungu kwa Binadamu
kwa hiyo tunaposhindwa kuitendea haki hii Kazi, Mjue kabisa Tunamkosea Mungu, tunaikwamisha Nchi, tunawaathiri Watoto na Wazazi na kwa dhambi hii lazima tutalipia.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa