Na. harunataratibu82@gmail.com
BARIADI-:MKUU WA Mkoa wa Simiyu,David Kafulila amewataka Wakufunzi wa sensa ngazi ya mkoa huo kwenda kutoa mafunzo bora kwa makarani watakaotumika katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu kwa lengo la kupata takwimu sahihi.
Rc Kafulila amesema hayo leo wakati akifunga mafunzo ya sensa kwa wakufunzi 205 ngazi ya mkoa huo ambao watakwenda kuwafindisha makarani wa sensa katika ngazi ya wilaya.
Amesema kwa kuwa wakufunzi hao wamepatikana kwa sifa zilizotakiwa ni matumaini yake makubwa pia makarani watakaokwenda kufundishwa na wakufunzi hao nao watakuwa Watu sahihi.
Amesema kuwa takwimu sahihi zitakazopatikana kwenye sensa ya mwaka huu zitaweza kutengeneza Dira yetu ya mwaka 2025 hadi 2050.
Pia amesema tafiti zinaonyesha kuwa takwimu zenye ubora zinachangia asilimia 1.5 ya pato la Taifa na hiyo ni kwa upande wa Uchumi.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa