Na. harunataratibu82@gmail.com
Kamati ya Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima(CMT) ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Elizabeth Gumbo imekataa kuyapokea madawati yaliyo tengenezwa chini ya kiwango wakati ikikagua Mradi wa vyumba viwili vya Madarasa katika Shule ya Msingi Mwalushu.
Kamati hiyo haikuridhishwa na Maendeleo ya utekelezaj Miradi katika Shule hiyo kutokana na kuonekana kuwa na dosari hususani Mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa ambapo madawati yake, yalionekana kutengenezwa chini ya kiwango na kwa kutumia mbao mbichi na zenye makovu mengi.
Mkurugenzi Mtendaji Bi. Elizabeth Gumbo alisema.
" Narudia kusema tena na tena, msicheze na pesa za Serikali, zitawapeleka pabaya, mbona wenzenu wametengeneza vizuri na wengine wapo Vijiji vya mbali, nyie shida IPO wapi? sasa basi haya madawati Siyataki na mkatengeneze Mengine yenye vigezo vinavyo takiwa"
Aidha Bi. Gumbo alimuagiza Mwalimu mkuu kuhakikisha ujenzi wa Mradi wa choo unaendelea haraka na ndani ya wiki mbili kuwe na Mabadiliko na Miundombinu yote ya choo isimame na shimo la Maji taka liendelee kuchimbwa.
Shule ya Msingi Mwalushu Ilipokea kiasi chaTsh. Milioni 53/= kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa na Ofisi na ujenzi wa Choo Cha Matundu 12..
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa