MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA HALMASHAURI (W) ITILIMA BI. ELIZABETH GUMBO AKIPOKEA MKATABA KUTOKA KWA AFISA KAZI KUTOKA OFISI YA WAZIRI MKUU SERA,URATIBU BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU KANDA YA MWANZA NDG. GOODLUCKY LUGINGA, KULIA NI MAKATIBU WA BARAZA.
|
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wameaswa kufanya kazi kwa kujituma na kuepuka vitendo vya ulevi wakati saa za kazi na ufanyakazi kwa mazoea ili kuwa mfano wa kuigwa katika jamii inayowazunguka
Akiongea na Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Afisa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu kanda ya Mwanza Ndg. Goodlucky Luginga alisema
“sisi kama wafanyakazi tunapaswa kufanya kazi kwa kujituma muda wote na vitendo vya ulevi wakati wa kazi ni mwiko na ni kosa la kuachishwa kazi hivyo aliwaomba wajumbe wa Baraza wakawapatie taarifa hiyo Watumishi wenzao wanao wawakilisha”
Akiainisha majukumu ya Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ndg. Luginga alisema yakuwa Mjumbe wa Baraza hilo lazima awe na uwezo wa kuchanganua mambo kwa ufasaha, kuchunguza chanzo cha tatizo kati ya Taasisi na Wafanyakazi anao wawakilisha na alisisitiza kwa kuainisha majukumu ya Baraza la Wafanyakazi ambayo ni kupanga mipango ya Halmashauri, kuimarisha mipango hiyo na kuwashawishi na kuwahimiza Wafanyakazi kufanya kazi, Kupokea mapendekezo ya mapato na matumizi ya Halmashauri”
Sanjari na hayo , Afisa kazi huyo aliwaomba Wajumbe kabla ya kuhudhuria Baraza wapite kwa wajumbe wanao wawakilisha ili kuweza kupata maoni yao, pia kuwapatia mrejesho wa Baraza ili waweze kutathimini kiasi cha maoni yaliyotekelezwa na ambayo hayajatekelezwa.
Baraza la Wafanyakazi lilikuwa chini ya Uwenyekiti wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Bi. Elizabeth Gumbo ambaye kabla aliongoza uundwaji upya wa Baraza kwa kuwasililisha majina ya wagombea kwa nafasi ya Katibu na Katibu msaidizi ambapo wajumbe walimchagua BI. Joyce A. Mhando Ambaye ni Afisa Utumishi kwa nafasi ya Ukatibu wa Baraza kwa kura 25 na Athony P. Masilu (afisa Mipango Msaidizi) kwa nafasi ya Ukatibu Msaidizi wa Baraza kwa kura 24.
Wakijadili Mapendekezo ya Rasimu ya Bajeti ya Mapato na Matumizi maeneo yasiyopata ruzuku na yanayo pata ruzuku mwaka 2020/2021 na Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2020/2021 hadi 2022/2023 wajumbe wa Baraza la wafanyakazi waliibuka na hoja zifuatazo
Akihoji kuhusiana na idadi ya maduka yaliyo orodheshwa kama chanzo Katibu wa CWT wilaya ya Itilima Ndg. Njile A. Lufasinza alihoji ya kuwa idadi ya maduka ni ndogo na kuomba idara husika ifanye utafiti ili kupata idadi kamili ya maduka ya nguo katika Halmashauri
Akijibu hoja hiyo Mkuu wa idara ya Mapato Ndg. Sile Sefu alisema ya kuwa idadi hiyo inatokana na idadi ya maduka yanayostahili kulipa leseni, kuhusiana na uanzishaji wa kituo cha Magari ya abiria katika Kata ya Luguru, Ndg Sefu alijibu ya kuwa.
“Tumekusudia kuanzisha kituo cha Magari ya abiria katika Kata Mwamapalala, ndiyo maana Chanzo hiki tumekiweka kwenye Rasimu yetu ya Bajeti kama chanzo cha Mapato.
WAJUMBE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WAKISIKILIZA KWA MAKINI MAELEZO YA MWENYEKITI WA BARAZA BI. ELIZABETH GUMBO (HAYUPO KATIKA PICHA
|
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa