Madiwani wa Itilima wakiwa katika kikao cha kwanza kwa cha Baraza kwa mwaka mpya fedha 2018/2019 |
Mkuu wa wilaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi ameitaka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Itilima kukamilisha kwa wakati Miradi yote ya Maendeleo iliyotengewa fedha.
Akitoa Taarifa za Serikali kwenye Kikao cha Baraza Madiwani la kwanza kwa mwaka mpya wa fedha 2018/2019, Mhe. Kilangi alisema “utekerezaji wetu wa Miradi ni mzuri na umeendelea kutujengea taswira nzuri mbele ya viongozi wetu wa Mkoa na Kitaifa, tusije kulegalega na kuchafua taswira ambayo imetughalimu kuijenga, ninaomba Miradi yote yenye fedha ikamilike kwa wakati”.
Vile vile Mhe. Kilangi alizungumzia suala la ukusanyaji wa Mapato na kuitaka ofisi ya Mkurugenzi kujiwekea Malengo ya Jinsi gani Halmashauri itafikia asilimia 81 ya makusanyo iliyowekwa kwa kila Halmashauri “ Mkurugenzi katika hili kaa na timu yako ya uongozi (C.M.T) muangalie ni jinsigani mtaunganisha nguvu kazi na kuyafikia malengo haya” alisema Mhe. Kilangi.
Sanjari na hayo Mhe. Mkuu wa Wilaya alizungumzia suala la Pamba hususani ugawaji wa Mbegu za pamba kwa wakulima. Zoezi ambalo limekamilika na aliwataka viongozi kushiriki kikamilifu kusimamia zao hili ambalo ndiyo zao Kuu la Biashara kwa Itilima.
Akimpongeza Mkuu wa Wilaya kwa kile alichoeleza kuhusiana na Pamba Diwani wa Kata ya Kinang’weli Mhe. Scania J. Luyombya alisema
”nikupongeze Mhe Dc kwani ni Viongozi wachache sana huonekana wakati wa maandalizi ya mwanzo ya kuwaandaa wananchi kwa ajili ya msimu Mpya wa kilimo cha pamba, wengi wao huonekana wakati wa mavuno”
Akitoa ufafanuzi jinsi ya kuepukana na utegemezi wa zao moja tu, Mhe Scania alisema “ Mhe. Mkuu wa Wilaya, wilaya yetu tumepata bahati ya kuwa na mazao mchanganyiko mengi sana, tumeshindwa kuyadhibiti tu na kuyafanya kuwa mapato na kupitia udhaifu huu, wajanja wanayavusha mazao yetu bila kutozwa ushuru na kwenda kuzinufaisha wilaya za Jirani.Tukijizatiti katika usimamizi tutaondokana na utegemezi wa pamba kama zao pekee la kiuchumi wilayani Itilima”
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Ndg. Kelisa Wambura alielezea shughuli zinazo tekelezwa na Ofisi ya Mkurugenzi kwa sasa ni ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi awamu ya pili ambao unaendelea vizuri.
Aidha Kaimu Mkurugenzi huyo alisema “ kwa sasa tupo katika maandalizi ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayo tarajiwa kujengwa katika Kijiji cha Nguno kilichopo katika kata ya Lagangabilili na baadhi ya vifaa vya ujenzi kama mawe na Mchanga vimeshaanza kupelekwa katika eneo la ujenzi.
Vile vile Ndg. Wambura alizungumzia maandalizi ya kuwapokea Wanafunzi wa Darasa la kwanza na Kidato cha Kwanza ambapo alisema kunauhitaji wa Vyumba 40 vya madarasa kwa shule za sekondari na vyumba 1635 kwa shule za Msingi zilizopo wilayani Itilima.
Kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani kwa mwaka huu mpya wa fedha 2018/2019 kilihitimishwa kwa kuhazimia yafuatayo ikiwemo utekelezaji wa miradi yote yenye fedha kwa wakati, ziara za kamati mbalimbali zifanyika kwa wakati sahihi na ukamilishaji wa miundombinu katika gulio la Lagangabilili ndani ya wiki Mbili
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa