Na. Haruna Taratibu
SEQUIP NOBORA.pdf
Mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Nobora unao tekelezwa na Mpango wa uboreshaji Elimu Kwa shule za Sekondari (SEQUIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia Sasa upo katika asilmia 96(%) za ukamilishaji
Mradi huu umekuja baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima kupokea fedha kiasi cha Tshs. Milioni 470/- na unatekelezwa katika Kata ya Nobora ambayo haikuwa na shule ya Sekondari.
Mpango huu wa SEQUIP una lengo la kuboresha mazingira ya kujifinzia Kwa watoto wa like ambao kihalisia wanapitia changamoto nyingi kufikia ndoto zao.
Mradi huo Kwa Sasa upo katika hatua ya umaliziaji Kwa fedha zilizo tengwa katika awamu ya Kwanza na unajumuisha Jengo la Utawala, vyumba vya Madarasa nane, Maabara za Sayansi tatu, chumba cha Komoyuta, Jengo la Maktaba na Vyoo.
Kukamilika Kwa mradi huu utatoa fursa kwa watoto wa kike kusoma katika mazingira mazuri yaliyo karibu na makazi Yao na kuondokana na adha waliyo kuwa wakipitia ya kwenda kupata elimu ya sekondari katika Kata za jirani za Luguru na Mbita.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa