Na. harunataratibu82@gmail.com
Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe. Njalu D. Silanga Leo ameshiriki zoezi la kukabidhi bodaboda tano kwa kikundi cha vijana cha bodaboda cha Kijiji cha Ndingho kilichopo katika Kata ya Mwaswale Wilayani Itilima.
Amikabidhi bodaboda hizo zenye thamani ya tsh. Milioni 12.25 Mhe. Mbunge aliwaasa vijana hao kutunza vyombo hivyo ili lengo la kujikomboa kiuchumi liweze kufikiwa.
Aidha Mhe. Njalu alisema " mnawajibika kutekeleza mashariti ya mkopo huu ikiwa pamoja na kulipakwa wakati marejesho ya mkopo, vile vile muwashawishi vijana wengine wajiunge katika vikundi, wasajiliwe na wawezeshe na w apate kujikomboa"
Kwa upande wa Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Mhe. Mboje Mhuli aliwaasa vijana hao kulejesha mkopo huo kwa wakati.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (W) Itilima Bi. Elizabeth Gumbo aliwapongeza vijana hao kwa kukidhi vigezo na kukopeshwa bodaboda hizo na kuwataka kutunza vyombo hivyo kwa umakini kwa sasa ni sehemu ya Akira Yao.
Vijana hao waliwekewa Lita tana za mafuta ya petroli na Lita Moja ya Oil pamoja na kukatiwa bima ILI waanze Kazi ya kujiingizia kipato pamoja na kurejesha marejesho ya mkopo huo.
Itilima ni miongoni mwa Wilaya zinazo tekeleza kwa vitendo sera ya kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuwainua kiuchumi Wanawake, vijana na jamii ya watu wenye ulemavu.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa