Na. harunataratibu82@gmail.com
Itilima imepokea kiasi Cha Sh. Bilioni 46.3/- Katika kipindi cha mwaka mmoja wa serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mama Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo Kugharamia Elimu bila ada.
Mapokezi hayo ya fedha yalielezwa na Mhe. Mkuu wa wilaya ya Itilima Mhe. Faidha S. Salim wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Nkoma ambayo nayo Mhe. Diwani wa Lata hiyo Mhe. Daudi Majaba alisema Nkoma imenufaika na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 500/-
Mradi wa maji unaotekeleza Kwa fedha za Uviko - 19 katika Kijiji ya Bunamala Mbugani, mradi huu ulipokea Zaidi ya sh. Milioni 400/- na utajumuisha vituo cya kuchotea mahi 11.
Akiainisha miradi iliyotekelezwa Wilayani kwake mhe. Faidha alisema katika sekta ya maji Itilima imeshapokea zaidi ya Sh. Bilioni 2.3/- kutoka katika bajeti Sh. bilioni 5/- na miradi inayotekelezwa itakapo kamilika mapema mwezi wa tano itapelekea upatikanani wa maji Kwa 74.5%, upatikanani Kwa Sasa ni 63%.
" Kunautekelezaji wa Mradi wa ziwa Victoria utakapo kamilika Itilima tutavuka matakwa ya Ilani ya CCM ya 85% za upatikanaji wa maji, Mradi huo wa ziwa Victoria utekelezaji wake umeanza na Tanki kubwa la Maji litajengwa katika kata ya Chinamili wilayani Itilima na kuhudumia Wilaya za Meatu na Maswa, kama Tanki linajengwa Itilima Nkoma itakosa Maji? Aliuliza Mhe. Faidha
Katika Sekta ya Umeme Mkuu wa Wilaya ya Itilima alisema Serikali ya Mama Samia imeitengea wilaya yake Sh. Bilioni 30.1 kupeleka umeme katika vijiji 57 vilivyo salia na mkandarasi yupo katika eneo la mradi, Mkandarasi ameisaini mkataba wa miezi 18 ya usimikaji wa miundombinu na usambazaji wa umeme.
Mradi wa ujenzi wa jengo la huduma ya Dharula (EMD) katika hospitali ya wilaya ya Itilima. |
Katika Sekta ya Afya wilaya ya Itilima imepokea bilioni 1.9 ambayo inatekeleza miradi mikubwa katika hospitali ya wilaya kama ujenzi wa jengo la huduma za dharula (EMD) ujenzi wa jengo la Upasuaji na wodi zake mbili,nyumba ya kuhifadhia maiti pamoja na Nyumba tatu za wahudumu wa Afya.
Mhe. Rais aliipatia Itilima kiasi cha Sh. Milioni 500/- za Tozo kutekeleza mradi ya ujezi wa kituo kipya cha Afya cha Kanadi katika Kata ya Migato, ambapo kukamili
Mradi wa ujenzi wa zahanati ya Kamado inayojengwa Katika Kijiji Cha mwanhunda baada ya Halmashauri kupokea fedha ya tozo kutoka serikali kuu kiasi Cha sh. Milioni 500. |
Pamoja na Milioni 300/ zitatumika katika ukamilishaji wa zahanati sita za Dasina, Laini, Nhobora, Nkololo na Bulolambeshi.
Vilevile Itilima ilipokea fedha kiasi cha Sh. bilioni 2. 9 Kwa ajili ya ujenzi was miundombinu katika sekta ya Kilimo na Mifugo fedha hizi zinajenga majosho katika Kijiji cha Habia na Ngeme na Ghala kubwa la kuhifadhia cha Kula na Maabara ya kupima cha kwa lengo la kudhibiti Sumu Kuvu katika mazao.
Mradi wa ujenzi wa Ghala la kuifadhia chakula linalojengwa katika kata ya Ikindio baada ya kupokea fedha kiasi Cha sh. Milioni 900/- kutoka serikali kuu, mradi huo utajumuisha maabara ya kupima mazao kuhakiki usalama wa chakula. |
Kuhusiana na Fedha za mradi wa Kunusuru kaya Maskini "Tasaf" katika kipindi cha mwaka mmoja, itilima imepokea kiasi cha Bilioni 2.1 Kwa ajili ya walengwa wa Tasaf na kupitia fedha hizo walengwa hai wamefanikiws kuibua miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya ufunguaji wa barabara na ujenzi wa Visima na kupitia fedha hizo Tasaf ninaenda kujenga madarasa na BwenI la watoto wakike katika Kijiji Cha Shishani.
"Kwenye Fedha zetu za Mapato ya ndani Kwa mujibu wa miongozo ya serikali za Mitaa inataka 40% ielekezwe katika Miradi ya maendeleo na Mpaka Sasa Halmashauri imeshatoa kiasi Cha Sh. Milioni 204 na zimejenga madarasa na vyoo na kulipa fidia eneo ambalo itajengwa stendi ya magari ya abiria " alisema Mkuu wa wilaya huyo
Vilevile halmashauri inaendelea kutoa 10% za mapato ya ndani Kwa ajili ya Mikopo ya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu na ndani ya mwaka mmoja vikundi 16 vimeshakopeshwa kiasi cha Sh. Milioni 96 .
Mradi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Ikindilo mradi huo unatekdleza Kwa mapato ya ndani ya Halmashauri baada ya kutengewa Milioni 25/- |
Sekta ya elimu ni miongoni mean sekta zilizo pokes fedha nyingi kiasi Cha zaidi ya Sh. Bilioni 3.16 katika kipindi Cha mwaka wa Fedha 2021 - 2022 na fedha hizo zilifumika katika uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu Sekondari na Msingi.
Miongoni mwa miradi ya Kihistoria ni Ile iliyopelekea itilima kutekeleza ujenzi wa vyumba 78 vya madarasa Kwa shule za sekondari na na vyumba nne vya shule Shikizi ndani ya miezi mitatu baada ya kupokelewa kiasi cha Sh. Bilioni 1.6 kutoka fedha za mapambano dhidi ya uviko.
Aidha siku za Karibuni Halmashauri ya Itilima ilipokea kiasi cha Sh. Milioni 470/- Kwa ajili ya ujenzi wa ya Kata ya Nhobora ambayo itakuwa n shule ya Wasichana na unaendelea
Katika fedha hizo Elimu Msingi ilipokea zaidi Milioni 900/- Kutoka katika taasisi mbalimabali za serikali, ikiwemo TEA, EP4R na kupitia miradi hiyo madarasa katika shule mbalimbali zilizo kuwa na changamoto za uchache wa Madarasa zimepa ikiewemo Mhunze na Ipilili Shule za Msingi pamoja na ujenzi wa Bweni katika shule ya Msingi Lagangabilili na ujenzi wa nyumba nne za walimu Ng'wang'wita.
Wanancha wa Kata ya Nkoma wakifuatilia Kwa makini hotuba ya Mkuu wa wilaya ya Itilima Mhe. Faidha Salim hayupo katika picha |
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa