Na. Haruna Taratibu
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Itilima leo limepitia taarifa ya hesabu za Mwaka wa fedha unaoishia Juni 30,2022 katika kikao hicho Wah. Madiwani walijikita katika Taarifa ya Mizania (Statement of Financial position), Taarifa ya Mapato na Matumizi (Statememt of Finencial Perfomance, Taarifa ya mabadiliko katika mali halisi za Halmashauri (statement of Changes in Net Asset na Mtiririko wa fedha (Cash Flow Statememt.
Wah. Madiwani wakifuatilia Kwa Makini wasilisho kutoka Kwa Mweka Hazina la Taarifa ya Hesabu za Halmashauri zilizo ishia Juni 30,2022 |
Akiwasilisha Taarifa Hiyo Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itilima, Mweka Hazina wa Halmashauri Bw. Essau Njawa alisema ya kwamba“Taarifa Hiyo imeandaliwa kwa kufuata viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta za Umma IPSASs, pamoja na Sehemu ya (iv) ya Sheria Na. 9 ya Fedha za Mamlaka ya Serikali za Mitaa ya Mwaka 1982 iliyo rekebishwa mwa 2000 kulingana na agizo Na. 31(3) la Memoranda za Serikali za Mitaa yam waka 2009.
Kulingana na wasilisho hilo Taarifa za Hesabu za Halmashauri ya Itilima kwa mwaka wafedha 2021/2022 zimejumuisha taarifa za kifedha za Makao Makuu ya Wilaya ya Itilima, na taarifa za kifedha za ngazi zote ikiwepo katika shule zote za Msingi na Sekondari, Hospitali ya Wilaya, vituo vya Afya , Zahanati na Vijiji Kutokana na Mizania ya Halmashauri taarifa zilizo ainishwa ni Mali za Muda Mfupi zenye thamani ya Shilingi Bilioni 7,902,039,693.00 ambapo fedha taslimu ikiwa Bilioni. 3.796,447,197.00
Huku fedha zilizoko kwa wadaiwa ni Bilioni. 1,857,331,144.00 huku vifaa vilivyo salia stoo vikiwa na thamani ya Tsh. Bilioni 2,248261,352.00.Aidha kwa upande wa mali za kudumu Halmashauri ina mali zenye thamani ya Tsh. Bilioni 28,020,352,516.00, mali hizo ni kama Ardhi, Majengo, Mitambo na Mashine, Kompyuta na vifaa vyake, samani za ofisi, magari, pikipiki na baiskeli na mashine za kukusanyia mapato.
Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Itilima wakifuatilia Kwa makini Mjadala wa Baraza maalumu la taarifa za hesabu za Halmashauri. |
Aidha kwa upande wa taarifa ya madeni ya muda mfupi, ina jumla ya Tsh. Bilioni 5,087,171,774.00 ikihusisha taarifa ya wadai wa Halmashauri ambao wanadai kiasi cha Tsh. Bilioni 1,780,353, 767.00 na fedha za Ruzuku ya shughuli za kawaida ambayo haikutumika kiasi cha Tsh. Bilioni 3.306,818,007.00
Taarifa ili hitimishwa kwa kuonyeza Mtiririko wa fedha ambazo Halmashauri imepokea na kulipa katika shughuli za uendeshaji, uwezeshaji na uwekezaji kwa mwaka mzima ambapo fedha iliyopokelewa ni Tsh. Bilioni 28,607,813,417.00 ambayo ilihusisha Mishahara, uendeshaji wa Elimu bila malipo, utekezaji wa miradi ya maendeleo na Huduma za Afya.
Katika kiasi hicho, fedha iliyo tumika ni Tshs. Bilioni 28, 111,749,564.00 huku fedha iliyotumika katika Uwezeshaji ikiwa ni Tshs. Milioni 250,676,529.00 na salio anzia kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Tshs. Bilioni 1,844,525,608.00 huku salio ishia kwa mwaka 2021/2022 likiwa fedha taslimu kiasi cha Tshs. Milioni. 654,369,047.00.
Diwani wa Kata ya Zagayu Mhe. William Kuzenza akichangia mada katika kikao maalum cha Baraza la kujadili taarifa za Hesabu za Halmashauri zilizo ishia Juni 2022. |
Akichangia kuhusiana na taarifa hiyo Diwani wa Kata ya Zagayu Mhe. William Kuzenza alipongeza uongozi kwa kusimamia matumizi na kupelekea Halmashauri kuwa na mali za Kudumu zenye thamani ya Zaidi ya Tsh. Bilioni 28/ pamoja na kuwa na Mizania ya fedha ainzia kiasi cha Tshs. Bilioni 1.8/= na Fedha ishia kiasi cha Zaidi ya Tshs Milioni 600/= kwa mujibu wa Mhe. Kuzenza Halmashauri ya Itilima imepiga hatua kubwa
Diwani wa Kata ya Luguru Mhe. Robert Jongela alishauri Uongozi kuweka utaratibu wa uwekezaji kwa siku za usoni ili Halmashauri iweze kupata fedha kupitia Hisa zitakazo wekezwa katika makampuni mbalimbali.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa