• MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
Itilima District Council
Itilima District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Sisi ni nani?
    • Dira na Dhamira
    • Taarifa ya Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango
      • Afya
      • Mifugo
      • Kilimo
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi
      • Sheria
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
    • Muundo
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Ujenzi
    • Leseni za Biashara
    • Umilikaji wa Ardhi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba Video
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi inayofadhiliwa na Wahisani
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea na Ujenzi
    • Maandiko ya Miradi
  • Zabuni
  • Uwekezaji
  • FFARS LINK

MADIWANI ITILIMA WAPITISHA SHERIA KUDHIBITI SUMU KUVU

Posted on: August 26th, 2022

Na.Haruna Tararibu

Baraza Maalum la Madiwani la  Halmashauri ya wilaya ya Itilima  limeridhia Kwa kauli moja uwepo wa Sheria ndogo za kuzuia na kidhibiti Sumu Kuvu wilayani humo.


Kabla ya majidiliano kuanza Mwanasheri wa Halmashauri Adv. Joshua Shayo alitoa ufafanuzi na umuhimu wa Sheria hiyo kuridhiwa na kupitishwa na Baraza, wakili Shayo  alisema.

Mwenasheria wa Halmashauri ya Itilima akiwasilisha mada ya Sumu Kuvu katika Baraza maalumu la madiwani

"Aina haja ya kuogopa uwepo wa Sheria hizi  na Wala hakuna lengo la kuzifanya ziwe chanzo cha mapato, lengo kubwa ni kuzisaidia jamii yetu izingatie hizi kanuni za Kilimo Bora na hata Yale yanayo onekana ni makosa ni yale matakwa 10 ya kanuni za kilimo bora kama kuandaa mashamba Kwa wakati, kupanda Kwa wakati, kutumia mbegu bora,


 kutumia viwatilifu Kwa usahihi, kuvuna Kwa wakati, kukausha mazao kwa njia zinazo kubarika hata kama ni za asili na njia Bora za usafirishaji mazao pamoja na suala Zima la uhifadhi wa mazao ili kuiepuka sumu kuvu"


Aidha mwanasheria huyo aliongeza ya kuwa kutokana na Halmashauri ya Itilima kuwa moja ya Halmashauri 20 nchini zilizopata mradi wa (TANIPAC) wa kudhibiti sumu kuvu, pamoja na ujenzi wa maghala na maabara, pia takwa moja wapo ni kuwa na Sheria ndogo ambazo zitasaidia kuielekeza jamii juu ya taratibu na misingi ya Kilimo bora ambazo zitasaidia kuondokana na majanga ya sumu kuvu.


Katika kikao hicho maalumu kulikuwepo na hali ya kutofautiana Kwa hoja miongoni mwa Wah. Madiwani  huku baadhi wakitaka kutokuwepo Kwa Sheria hiyo sababu italeta athari wananchi.


Akichangia hoja kuhusiana na mada ya Sumu Kuvu diwani wa Kata ya Zagayu Mhe. Wiliamu Kuzenza alisema.


" makosa huwa yapo na ili mwanadam aweze kujirekebisha ni lazima umtungie sheria, hizi Sheria ni kwa ajili ya kuwakinga wetu na athari, ndio maana mradi ukaletwa hapa, Kwanza tulipewa elimu tukapiga makofi na posho tukapewa , wataalamu wakaenda Kwa wananchi na wananchi wamepokea cha msingi sisi tusiwe na pingamizi zaidi ya kuzipitisha kanuni hizi ili ziwalinde watu wetu.


Kwa upande wa Diwani wa Lagangabilili Mhe. Dotto Adam alisisitiza ya kwamba Sheria hizi zitaleta kilio kikubwa Kwa wananchi wetu na kutaka adhabu zilizo pendekezwa kutozwa kama kiasi kisichozidi Tshs. Laki tatu au kifungo kisichizidi miezi sita zipunguzwe Kwa fedha ianzie elfu 20/ na isizidi elfu 50 na elimu iendelee kutolewa Kwa miaka miwili, baada ya hapo utekelezaji wa Sheria hizi ufuatie.

Wah. Madiwani wakifuatilia Mjadala katika Baraza Maalumu la kujadili mada ya Sumu kuvu

Diwani wa Kata  ya Luguru Mhe. Robert Jongela alikua na Mtazamo tofauti na kuwaomba Wah. Madiwani kupitisha Sheria hizi  Kwa lengo la kunusuru maisha ya watu na Biashara ya kimataifa, Diwani huyo alisema.


"Mradi huu wa kudhibiti sumu kuvu (TANIPAC) unatekelezwa katika Halmashauri 20 tu ,Itilima  ikiwepo Kati ya Halmashauri 184 Kwa hali hii Kwanza inaonyesha uzito wa Mradi huu na kama haitoshi kupitia mradi huu Mhe. Rais ametuletea Milioni 900/- za ujenzi wa Ghala la kisasa la kutuzia mazao, likihusisha uwepo wa maabara ya kupimia sumu kuvu hii pekeake inaashiria kuwa serikali imekusudia kuwanusuru watu wake"


Mhe. Jongela alitolea mfano wa kipindi ambacho mahindi ya Tanzania yalizuiliwa kuingia Kenya baada ya kubainika kuwa Yana sumu kuvu na baadae  kuteketezwa huu utaratibu ungekuwepo mapema wafanyabiashara wasinge safirisha mahindi ya aina hiyo na kuepuka hasara"


Akitoa mtazamo wa Serikali Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Faidha S. Salim alisema ya Kwamba ni muhimu kuwa na Sheria na tuwaelimishe watu wetu kupita katika hizo Sheria, na wasiachiwe wataalamu pekeyao na ndio maana tulipewa mafunzo, wananchi wasipo banwa kisheria maana yake tunaenda kudidimiza afya zao baadaye tutakuwa tunaongoza wananchi wenye afya mbovu.


Mjadala ulihitimishwa  na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itilima Mhe. Daudi Nyalam kwa kuwakimbisha Wahe. Madiwani kuwa hakuna Taasisi bila kanuni hata huu mradi huwezi kufikia malengo bila kanuni cha msingi Wah. Madiwani twendeni tukawe sehemu ya kutoa elimu na siyo sehemu ya kutetea sheria isitekelezwe.


Halmashauri ya Itilima ni miongoni mwa Halmashauri  zinazo tegemea kilimo kwa zaidi ya asilimia 98, na Kati ya Halmashauri 20 zinazo tekeleza mradi wa TANIPAC wa kuzuia na kudhibiti sumu kuvu kwa lengo la kutoa elimu zaidi na kulinda afya za wananchi na kiwaepusha na hasara katika biashara ya mazao.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA WILAYANI ITILIMA October 30, 2021
  • Tangazo Kwa Watumishi Wapya Wanao endelea kuwasili Wilayani Itilima July 03, 2022
  • "Tutaukaribisha Mwenge wa Uhuru Wilayani Itilima tarehe 9/7/2022 tutaupokea katika Viwanja vya Ushirika, Nyamalapa na mkesha utakuwa katika viwanja vya Halmashuri ya Wilaya ya Itilima Wananchi wote, Wafanyakazi tuungane katika makaribis July 07, 2022
  • "Tutaukaribisha Mwenge wa Uhuru Wilayani Itilima tarehe 9/7/2022 tutaupokea katika Viwanja vya Ushirika, Nyamalapa na mkesha utakuwa katika viwanja vya Halmashuri ya Wilaya ya Itilima Wananchi wote, tuungane katika kuukaribisha Mwenge July 06, 2022
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • TUME YA TAIFA YA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI YAPIMA NA KUKABIZI HATI ZA VIJIJI 25 VILIVYOPO KANDO YA POLI LA AKIBA LA MASWA

    June 30, 2024
  • BARAZA LA ARDHI ITILIMA SASA RASMI BAADA YA KUAPISHWA KWA WAJUMBE WA BARAZA

    June 26, 2024
  • KUNA MAISHA BAADA YA UTUMISHI WA UMMA

    June 20, 2024
  • MWALIMU TIMIZA WAJIBU WAKO WA MSINGI KWA AJILI YA NCHI YAKO, WAZAZI WA TANZANIA NA WATOTO KUZIFIKIA NDOTO ZAO

    June 20, 2024
  • Angalia Zote

Video

BARAZA LA MADIWANI LA MADIWANI LA WILAYAYA ITILIMA LAUFUNGA MWAKA WA FEDHA WA 2020 - 2021
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Business License
  • Procedure for Provision of Buliding Permit
  • https://www.nbs.go.tz/index.php/en/census-surveys/population-and-housing-census/802-sensa-ya-watu-na-makazi-ya-mwaka-2022
  • Land Ownership

Tovuti Mashuhuri

  • Simiyu Regional Commissioner's Office
  • President's Official Website
  • Local Government Revenue Collections Dashboard
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Salary Slip Self Service
  • FFARS LINK
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    DED - ITILIMA

    Sanduku la Posta: 308 BARIADI

    Simu: +255 28 29 863 29

    Simu: 028 29 863 28

    Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa