Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ahidi kutoitupa Familia ya Mkurugenzi wa Itilima Marehemu Mariano Mwanyigu.
Mhe. Mtaka alitoa ahadi hiyo katika mazishi ya marehemu Mwanyigu yaliyo fanyika katika viwanja vya Kanisa katoliki vilivyopo katika kijiji cha Luhololo Wilayani Njombe.
"Nisingependa kusikia Mjane wa Marehemu anaanza kuangaika kufuatilia mirathi ya Marehemu Mume wake wakati bado tupo kwenye utumishi wa umma na kuna umoja wa Wakurugenzi 184 Nchi nzima, Marehemu alikuwa wa 185 ambao wanaweza kufanya jambo" alisema Mtaka.
Aidha Mtaka aliwataka wananjombe na viongozi wengine kujifunza kupitia Marehemu Mwanyigu kwa kufanya mambo kwa umakini na kuamini kile unachokifanya
" Mwanyigu alifanya mambo makubwa sana katika taaluma yake ya Ualimu na alijitengenezea mtandao kupitia taaluma hiyo, halikadharika katika Ukurugenzi wake alifanya hivyo, hakika sisi kama Wanasimiyu tutamkumbuka daima Mwalimu Mwanyigu " alisema Mtaka
Hata hivyo Mhe. Mtaka alitoa tahadhari kwa wana familia kuhusiana na mirathi ya Marehemu kwa kusema "Mirathi ya Marehemu Mwanyigu na ya Mjane wa Marehemu na watoto wake, haiwahisu ndugu wa mbali wala wa karibu labda waamue kuwapa"
Marehemu Mwanyigu alizaliwa mwaka 1964 Wilayani Njombe alihudumu kama mwalimu katika shule ya Sekondari ya Wavulana Songea, kabla ya kuhamia Shule ya Sekondari Njombe ambapo alihudumu kama makamo mkuu wa Shule, baadaye Marehemu alihamia katika shule ya sekondari J.J. Munga kama Mkuu wa Shule.
Mwaka 2015 Marehemu Mwanyigu aligombea Kuteuliwa kupitia CCM kuwa Mgombea wa Ubunge katika Jumbo LA Njombe Mjini lakini kura hazikutosha, kwa jitihada zote za kutaka kuwatumikia wananchi Rais wajamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Mgufuri alimteua kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Itilima ambapo paka mauti yanamkuta alikuwa Mkurugenzi wa Itilima.
#tutakukumbukadaima
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa