Na. harunataratibu82@gmail.com
Kamati ya Siasa Mkoa wa Simiyu ikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti ambaye ni Mneki wa Mkoa, Mhe. Gungu Silanga yaupongeza Uongozi wa Wilaya ya Itilima kwa kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa Miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa Wilayani humo.
Kamati hiyo ilifanya ziara katika Kata za Ikindilo, Mwamtani, Sagata, Ndoleleji na Mhunze na kuukagua Miradi ya Vyumba vya Madarasa 17, Madarasa manne katika Shule ya Sekondari Ikindilo, Madarasa mawili katika Shule ya Sekondari Mwamtani, Madarasa matano katika Shule ya Sekondari Laini, Madara mawili katika Shule ya Sekondari Ndoleleji na Madarasa manne katika Shule ya Sekondari Madilana.
"Itilima katika suala la utekelezaji wa Miradi mmekuwa mkiitendea haki Ilani ya chama chetu kikamilifu, kitu ambacho ni muhimu hapa ni kuhakikisha Madarasa haya yanakamilika kwa 100% ifikapo tarehe iliyopangwa na watoto wetu wa kidato Cha kwanza waingie Shule zitakapo funguliwa" alisema Mhe. Silanga
Aidha kwa upande wa katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu Ndg. Innocent Nanzaba alisisitiza ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba hivi vya Madarasa uendane na ubora na matumizi sahihi ya Fedha.
Ujenzi wa vyumba vya Madarasa kwa Wilaya Itilima umefikia hatua ya ukamilishaji Kazi ndogo ndogo ili kukabidhi Madarasa hayo kwa mujibu wa tarehe ya mwisho iliyopangwa.
Itilima Ilipokea fedha kiasi cha Tsh. BILIONI 1.64 kutoka Serikalini kwa lengo la kujenga Madarasa 78 ya shule za Sekondari na manne ya shule shikizi
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa