Na. harunataratibu82@gmail.com
Kamati ya Fedha na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima yafanya ziara na kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo yenye thamani ya Sh. Bilioni 1.89. katika Kata ya Mhunze, Migato, Ikindilo na Lagangabilili.
Ziara hiyo ilikagua Miradi ya Elimu yenye thamani ya Sh. Milioni 240/= ikihusisha Miradi ya ujenzi wa vyumba vinne vya Madarasa na Ofisi katika Shule ya Msingi Madilana na Shishani vyenye thamani ya Sh. Milioni 80/= .
Aidha kamati ilikagua Mradi wa ujenzi wa vyumba vinne vya Madarasa na Ofisi mbili katika Shule ya Sekondari ya Chinamili vyenye thamani ya Sh. Milioni 80/=, pamoja na Ujenzi wa Mradi wa Bweni la watoto wa kike katika Shule ya Msingi Lagangabili uliyo pata ufadhili wa kiasi Cha pesa Sh. Milioni 75/= ujenzi ukiwa katika hatua za awali.
Hata hivyo katika Miradi hiyo ya Elimu, wasimamizi wa Mradi wa Shule ya Msingi Shishani na Shule ya Sekondari Chinamili walitakiwa kuhakikisha wanamaliza Miradi hiyo kwa haraka kutokana kuwa nje ya muda wa kukabidhi
"Hakikisheni mnamaliza miradi hii haraka sababu mpo nje ya muda wa kukabidhi" Mhe. Daudi Nyalamu Mwenyekiti Wa Halmashauri.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Itilima Bi. Elizabeth Gumbo aliwataka wasimamizi wa Mradi wa Shishani na Chinamili kuongeza Mafundi ili kukamilisha Mradi huo kwa haraka.
Katika miradi ya Afya, Kamati ilitembelea mradi wa ujenzi wa Kituo Cha Afya Cha Kanadi ambapo hivi karibu Mradi huo ulipata fedha kiasi cha Sh. Milioni 250/ ujenzi ukiwa katika hatua za awali huku Mhe. Nyalamu aliwataka Wananchi wa Kata ya Migato kuchangia nguvu Kazi na kuleta Mchanga, Mawe na Kokoto.
Aidha Mhe. Nyalamu aliwapa muda wa siku saba wa kuonyesha ushirikiano Wananchi wa Kata ya Migato kabla ya kuamua kuhamisha Mradi huo na kupeleka sehemu nyingine.
Wakiwa katika Hospitali ya Wilaya, kamati iliridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Wodi tatu zilizo tengewa kiasi Cha Sh. Milioni 500, ikihusisha Wodi ya watoto, Wodi ya Wanawake na Wodi ya Wanaume, huku Wodi ya watoto na Wanaume ikiwa katika hatua za Umaliziaji.
Kamati ilipata fursa ya kutembelea Mradi wa ujenzi wa Ghala la kuhifadhia Chakula, wenye gharama zaidi ya Sh. Milioni 900/ uliyofadhiliwa na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Chakula na kutekelezwa na kampuni ya ujenzi ya Nice (Nice Engineering & Construction Co.) na utahusisha Ujenzi wa Ofisi na Maabara, ujenzi wa Ghala, ujenzi wa eneo la kukaushia Mazao,Vyoo na uzio.
Wilaya ya Itilima sasa ipo mbioni kuondoka na neno "Wilaya changa" ndani ya kipindi kifupi kijacho kwani huduma zote muhimu zitapatikana ndani ya Wilaya, na hii ni kutokana na miradi kikubwa Inayo tekelezwa na itakayo enda kutekelezwa muda si mrefu.
Tunakila sababu ya kusema ahsante Serikali ya Awamu ya Sita chini Mama Samia Suluhu Hasani kwa kuamua kutatua changamoto za huduma stahiki kwa Wananchi wa Itilima na Wanaitilima tunasema Ahsante sana Mama.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa