Na. Haruna Taratibu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Yahaya Nawanda amemuhakikishia Balozi wa Pamba Nchini Mhe. Aggrey Mwanri kuwa Itilima inaenda kuzalisha Tani 130,000 za pamba katika msimu huu wa kilimo.
Mhe. Nawanda aliongea hayo katika mafunzo maalumu yaliyo wahusisha Wakuu wa Idara na Vitengo,Maafisa Ugani, Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji, Wenyeviti na Makatibu wa Amcos wote wilayani Itilima.
Aidha Mhe. Nawanda alisema ya Kwamba Tanzania Imeweka malenga ya uzalishaji wa Tani 1,000,000 za Pamba katika hayo Malengo asilimia 50(%) inatakiwa kuzalishwa Mkoani Simiyu na Itilima ikitakiwa kuzalisha Tani 130,000 ilikufikia lengo la Mkoa la kuzalisha Tani 500,000.
Mhe. Nawanda aliwakumbusha Maafisa ugani ya kwamba
"Tulikubaliana maafisa Ugani wote wa Mkoa wa Simiyu lazima wawe na Ekali Moja za pamba, Mimi kama Afisa Ugani Mkuu nimelima Ekali 5 za pamba na hii italeta muamko Kwa wananchi wetu kujifunza Kwa vitendo njia Bora za kilimo katika mashamba yetu"
Mhe. Nawanda alisema tulisha kubaliana na Mkuu wenu wa Wilaya, Mkurugenzi na Afisa Ugani wa Wilaya kuzalisha Tani 130,000 katika Msimu Huu wa Kilimo na lazima zipatikane hizo Tani.
Kuhusiana na upungufu wa Tani 45 za Mbegu za pamba uliyo wasilishwa na Afisa Ugani wa Wilaya Ndugu Mateso Kiswanu, Mhe. Nawanda alimpigia Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania na Kuahidi kiasi hicho Cha Mbegu kitawasili Itilima ndani ya Siku Mbili.
Mhe. Nawanda alimaliza Kwa kusema ya Kwamba
"Tukizalisha sana, tutapata sana, tukipata sana, tuchangia maendeleo sana, tutabadilisha hali zetu za maisha, tutajenga nyumba Bora,tutanunua vyombo vya usafiri, tutasomesha watoto wetu, tutakuwa na Chakula cha kutosha, familia zetu zitaboreka na haya ndio malengo ya serikali ya awamu ya Sita.
Balozi wa Pamba Nchini Mhe. Aggrey Manri alisema ya Kwamba Mhe. Mkuu wa Mkoa madaraka ulonayo yanaweza kutumika viziri na kuleta tija katika zao pamba
Aidha Mhe. Mwanri alisema kuwa Serikali kupitia Bodi ya pamba ni Mwekezaji Kweli na tukifanya Bidii hatatupa vitu vinne ambavyo ni Malighafi, Uchumi, Ajira kwa vijana wetu na Mapato ya Serikali
Semina hii inayo ratibiwa na Bodi ya Pamba Tanzania huu ni Msimu wa Pili kifanyika na imewaza kuleta hamasa kubwa katika zao la pamba na Kwa siku ya Leo ilifanyika Makao makuu ya Wilaya ya Itilima na Katika Kijiji Cha Chinamili na Itaendelea Kesho katika Kata ya Mwamtani
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa