Na. harunataratibu82@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akikabidhiwa cheti na Mwenyekiti wa Halmashauri (W) Itilima Mhe. Daud Nyalamu kama ishara ya kutambua jitihada zake katika kisimamia Mkoa kitaaluma
|
Mkuuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila amewapongeza walimu wa Halmashauri ya Itilima Kwa kuongeza ufaulu katika mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne, kidato Cha pili,darasa la saba na la nne.
Mhe. Kafulila alitoa pongezi hizo katika hafla maalumu ya kuwapongeza walimu wa itilima Kwa kuongeza ufaulu kwa asilimia 6(%) na kuwa na 96% Kwa matokeo ya kitaifa Kwa shule za Sekondari na asilimia 90 Kwa matokeo ya kitaifa Kwa shule za Msingi.
Mhe. Kafulila aliupongeza uongozi wa Wilaya na wadau wa elimu wilayani humo Kwa kuandaa hafla ya kutambua mchango wa Mwalimu na kutoa motisha Kwa walimu kwani tukio hili litajenga shauku ya kufanya vizuri zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akimkabidhi cheti Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Faidha S.Salim kama ishara ya kutambua jitihada zake katika kisimamia Elimu
|
" kuongeza ufaulu Kwa asilimia sita na kuwa na ufaulu wa asilimia 96 (%) Kwa Sekondari na asilimia 90 Kwa Elimu Msingi Kwa Itilima na wilaya zingine ndiyo kumeufanya Mkoa wa simiyu kushika nafasi ya tatu kitaifa Kwa matokeo ya 2020 - 2021
Aidha Mhe. Kafulila alisema kuna kila sababu ya kuwapongeza walimu wetu kwa matokeo haya Itilima na Wilaya zingine zimeufanya Mkoa kushika nafasi ya tatu kitaifa na hii ni hatua kubwa kwa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Halmashauri (W) Itilima Mhe. Daudi Nyalamu kama ishara ya kutambua jitihada zake katika kisimamia taaluma |
"Unaposhika nafasi ya tatu kitaifa sisuala dogo ukizingatia changamoto tulizonazo kama Mkoa na maeneo yetu Kwa asilimia zaidi ya 90 ni Vijiji na miundombinu yetu ukilinganisha na wengine, Kwa kweli tunakila sababu ya kuwapongeza Walimu wetu kazi nzuri wanayofanya.
Mhe. Kafulila alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan Kwa kiasi kikubwa kutachochea hali ya kufanya vizuri katika elimu Kwa kutuletea Fedha kiasi cha Sh. Bilioni 7.6 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa 380.
"Kwa uwekezaji huu wa Mama katika elimu hatutaki kuona upuuziaji wa elimu na naiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya kufuatilia utoro rejareja wa wanafunzi na wazazi wanao waozesha wanafunzi"
Mhe. Kafulila aliagiza
Kwa upande wa Mkuu wa ya Itilima Mhe. Faidha S. Salim alielezea namna wilaya ilivyo jipanga katika kutatua changamoto zinazo ikabili sekta ya elimu na kuahidi kuandaa Harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya madarasa na nyumba za walimu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (W) Itilima Bi. Elizabeth Gumbo kama ishara ya kutambua jitihada zake katika kisimamia Idara ya Elimu
|
Akiwasilisha taarifa yautekelezaji Kwa sekta ya elimu, Mkurugezi mtendaji Bi. Elizabeth Gumbo alisema ya kwamba kama Halmashauri wameshaanza kutatua baadhi ya changamoto zinazo ikabili sekta ya elimu Kwa kutenga fedha kutoka katika mapato ya ndani na kizielekeza katika ujenzi wa madarasa.
Katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa aliwatunuku vyeti na Pesa kwa walimu waliyo fanya vizuri, wadau wakubwa wa elimu wakiongozwa na Mzee Katani Ndabagija na Viongozi wa Wilaya wakiongozwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Itilima na mwenyekiti wa Halmashauri ya Itilima alimkabidhi Mhe. Kafulila Cheti kama ishara ya kutambua jitihada za Mkuu wa Mkoa.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa