Na. harunataratibu82@gmail.com
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi - Afya Mhe. Festo Dugange ameupongeza Uongozi wa Wilaya ya Itilima kwa utekelezaji Mradi wa vyumba vya Madarasa uliozingatia viwango na ubora na thamani ya Fedha kuonekana
Akikagua Mradi wa vyumba viwili vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Idoselo Mhe. Dugange alisema
"Hakika mmezitendea haki fedha za Mpango wa Taifa wa Maendeleo na Mapambano dhidi ya Uviko 19" na hili itakua mme mthibitishia kwa vitendo Mhe. Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ya kwamba Itilima hamtakuwa na chaguo la pili kwa watoto wetu wanaotarajiwa kuanza kidato cha kwanza hapo mwakani"
Kwa hatua mliyofikia ya asilimia 90 ya ujenzi wa Madarasa Wilaya Mzima nauhakika mpaka tarehe 30/12/2021 mtakua mmekamilisha kwa asilimia 100, alisema Mhe. Dugange.
Akielezea changamoto iliojitokeza wakati wa utekelezaji wa Miradi hii Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Faidha Suleiman Salim alisema
" Mhe. Naibu waziri tulipokea fedha za Miradi hii tukiwa tunaelekea katika kipindi Cha kilimo na kutokana na Mazingira yetu vyombo vya usafiri ni matrekta na kipindi hiki yalikuwa mashambani, tukajikuta tupo katika changamoto ya kufikisha vifaa vya ujenzi katika maeneo husika.
Akijibu ombi la Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe. Njalu D. Silanga la kuomba kupatiwa usafiri kwa matumizi ya Idara ya Ujenzi Mhe. Dugange alisema kuwa kabla ya mwezi Mei, 2022 Itilima itapokea magari mawili Moja ni gari la kubebea wagonjwa na lingine litatumika kwa ajili ya ufuatiliaji wa Miradi.
Sanjari na hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Bi. Elizabeth Gumbo alimuomba Mhe. Naibu waziri kuendelea kuangalia Itilima kwani bado inachangamoto katika sekta ya Afya hususana uchache wa vituo vya kutokea huduma ya Afya na uchache wa Watumishi kwa kada ya Afya halikadharika uchache wa miundombinu kwa Shule za msingi.
Itilima Ilipokea fedha za Mpango wa Taifa wa Maendeleo na Mapambano dhidi ya Uviko 19 kiasi cha Tsh. BILIONI 1.64 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa 78 kwa Shule za Sekondari na vyumba vinne vya Madarasa ya shule shikizi na ukamilishaji wa Miradi hii itawezesha wanafunzi 4806 kuanza kidato cha kwanza kwa pamoja hapo januari, 2022.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa