Na. Haruna Taratibu
Halmashauri ya Wilaya ya Itilima katika kipindi cha mwezi Oktoba - Novemba imepokea fedha kiasi cha Tshs. Milioni 928.25 kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa Tiba, ujenzi wa miradi ya Afya, Elimu Msingi na Elimu Sekondari Kwa lengo la kuboresha na kisogeza huduma hizo karibu na wananchi.
Akiwasilisha taarifa ya mapokezi ya fedha hizo katika kikao cha Baraza la Madiwani robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Itilima Bi. Elizabeth M. Gumbo alisema
"Mhe. Mwenyekiti napenda kutoa taarifa katika Baraza lako kuwa Katika kipindi cha mwezi Oktoba na Novemba 2022 Halmashauri yako Imepokea Kiasi cha Tshs. Milioni 928.25 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba Katiba katika Hospitali ya Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati, na ujenzi miradi ya Afya, Elimu Msingi na Sekondari"
Aidha Bi. Gumbo aliainisha Mchanganuo wa hizo fedha kiasi cha Tshs. Milioni 300/- zimetengwa katika Kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa Tiba, Milioni Kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya, milioni 150/- Vituo vya Afya na Milioni 50 katika zahanati, na kiasi cha Tshs. Milioni 50 kimetengwa kumalizia maboma ya wagonjwa wa Nje katika zahanati ya Ng'walali, Isagala na Kidula na Jumla ya fedha zilizo tengwa ni Tshs. Milioni 350/
Kwa upande wa Elimu Sekondari Halmashauri imepokea kiasi cha Tshs. Milioni 200/- fedha hiyo itaenda kujenga vyumba vya Maabara maabara Sita, kimoja Kwa Kila shule ya Sekondari iliyo kusudia ambapo ni Shule ya sekondari Mahembe, Ndoleleji, Bunamhala,Madilana,Sagata, na Lung'wa ambapo Maabara hizo zote zitagharimu Tshs. Milioni 180/- na TShs. Milioni 20 itakamilisha ujenzi wa Bweni katika shule ya sekondari Lagangabilili
Vilevile kiasi cha Tshs. Milioni 378. 25 zimepokelewa Kwa ajili ya ujenzi wa Miradi ya Elimu Msingi ikiwemo ukamilishaji wa vyumba vya Madarasa 12 katika shule za Msingi sita ikiwemo shule ya Msingi Manasubi vyumba 2, Mwamalinze vyuma 2, Ntagwasa Vyumba 2, Lali vyumba 2, Mwakimisha vyumba 2 na Pijulu vyumba 2, vyumba vyote vitagharimu Tshs. Milioni 150/-
Katika hizo fedha kiasi cha Tshs. Milioni 22 kujenga matundu 20 ya vyoo, Matundu 10 katika Kituo shikizi cha Mwabulugu na Matundu 10 mengine katika kituo shikizi cha Mwazimbi.
Milioni 200/- itatumika kukamilisha Maboma 8 ya nyumba za Walimu, Maboma 2, katika shule ya Msingi Ngh'omango na Boma moja katika shule za Msingi ya, Ntagwasa, Nyantugutu, Mwamalize, Ipilili, Mahembe na Kidula ambapo Kila Boma limetengewa Tshs. Milioni 25/-
Sisi kama Wanaitilima tunaishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan Kwa kudhihirisha dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo wanaitilima kabla ya mapokezi ya Tshs. Milioni 928.25 katika mwezi huu wa Novemba, Julai - Septemba 2022 Itilima ilipokea kiasi cha Tshs. Milioni 540 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa 17 na tena ikapokea zaidi ya Milioni 300 Kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Tasaf.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa