Na, Haruna Taratibu
Wajumbe wa Kikosi kazi ya cha ufuatiliaji wa mapato cha Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakiratibu na kufuatilia zoezi zima la uvunaji wa Samaki katika Bwawa la Sawida.
|
ITILIMA KUJIIMARISHA KIUCHUMI KUPITIA "SAMAKI"
Halmashauri ya Wilaya ya Itilima imeanza zoezi la uvunaji wa Samaki waliyopandwa katika Mabwawa matatu yaliyopo wilayani humo, huku bwawa la sawida likitoa kilo 944 za Samaki katika uvunaji wa awali.
Akielezea Chanzo hiki cha Mapato Mkuu wa Idara ya Mapato Ndg. Sile Salmin Seif alisema
“Uvunaji huu wa samaki unaelekea kuwa chanzo madhuti cha mapato wilayani Itilima, tumeshavua mara tatu katika bwawa la Sawida na tumepata Zaidi ya kilo 900”
Aidha, ndg. Sile alisema kuna uwezekano wa kupata Zaidi ya Milion 20 kwa bwawa moja na Tuna mabwawa 04 yenye Samaki.
Itilima ilibahatika kupata Vifaranga 32,000 mchanganyiko kutoka Chuo cha Utafiti wa Samaki (TAFILI) cha Nyegezi na kuwapandwa, ambapo katika bwawa la Mwamapalala kulipandwa Vifaranga aina ya Sato 7000, bwawa la Sawida lilipata Vifaranga aina ya Sato 5000, huku Bwawa la Habiya kulipandwa vifaranga aina ya Kambale mumi 20,000.
Akitolea ufafanuzi wa chanzo hiki cha Mapato Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Kiraba Msoke alisema
“kwa jinsi tulivyo anza zoezi hili la uvunaji tunapata imani kuwa tunaweza kuwa na chanzo mbadala cha mapato mbacho itilima inaweza kujivunia hapo siku za usoni”
Aidha Dkt. Msoke alibainisha malengo mahususi ya Mradi huu mbali na Halmashauri, Serikali ya kijiji na Jumuiya za Watumiaji maji kupata mapato yatokamayo na Samaki vilevile Mradi utaimalisha hali ya afya na Lishe kwa wanaitilima.
Kwa lengo la kuufanya Mradi huu unakuwa ndelevu, Dkt Msoke alibainisha kuwa usafi wa mara kwa mara katika mabwawa haya utakuwa unafanyika, vile vile kwa kushirikiana na Watu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii watahakikisha wananchi wanapata elemu ya kutosha ya utunzaji wa vyanzo hivi ikiwa pamoja na kutoa ulinzi kwa maeneo haya dhidi ya vitendo uchungaji wa Mifugo kandokando vyanzo hivi na Uvuvi haramu.
Zoezi la uvunaji wa samaki katika bwawa la Sawida linaendelea na litafanyika mara nne kwa Mwezi na mipango ya kuanza uvunaji katika mabwawa yaliyo salia ya Mwamapalala, Habiya na Mwalushu, ipo katika hatua za mwisho.
Wananchi wakiwa katika mwalo wa bwawa la sawida baada ya kununua Samaki
|
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa