Na. Haruna Taratibu
Halmashauri ya Itlima Kwa mwaka wa Fedha 2021 - 2022 ilikisia kukusanya kiasi cha Tsh. Bilioni 1,487,035,716/-hadi Juni 2022 ilikuwa imekusanya kiasi cha Tsh 1,576,326,237/- kiasi ambacho ni sawa na asilimia 106 (%).
Kwa mujibu wa miongozo na kanuni zinazo ongoza serikali za mitaa zinahitaji makusanyo ya mapato ya ndani ukiondoa mapato lindwa, asilimia 40 (%) ya mapato huelekezwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na asilimia 10 (%) hutolewa kama mikopo Kwa vikundi vya wanawake (4%) na Vikundi vya vijana (4%) na jamii ya watu wenye ulemavu (2%)
Hivyo basi Halmashauri ya Itilima Kwa mwaka 2021 - 2021 kiasi cha Tshs. Milioni 219,514,350/- kilipelekwa kutekeleza miradi nane ya maendeleo na kiasi cha Tsh. Milioni 123,500,000/- kilitolewa kama mikopo Kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu.
Katika miradi iliyotekeleza ni pamoja na kulipia fidia eneo la Stendi kiasi cha Tsh. Milioni 13,900,000/ kilitumika sambamba na Tsh. Milioni 24,600,000/ kilitumika kujenga miundombinu ya stendi.
Vilevile Halmashauri itumia kiasi cha Tsh. Milioni tano kukamilisha mradi wa bweni katika shule ya sekondari Itilima na Milioni 20,000,000/ zilitumika kukamilisha ujenzi wa Bwalo katika shule ya sekondari Lagangabilili.
Halmashauri ilitumia kiasi cha Tsh. Milioni 50/- katika ukamilishaji wa Madarasa matano katika shule ya Msingi longalambogo madarasa wawili, shule ya msingi Chinamili Madarasa mawili na darasa moja katika while ya Msingi Ikindilo.
Katika kutatua changamoto za upatikanani wa huduma za afya katika Kijiji cha Kidula halmashauri ilipeleka kiasi Cha Tsh. Milioni 30/ za mapato ya ndani.
Katika mchakato wa kuyainua makundi maalumu Halmashauri ya Itilima chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mtendaji Bi. Betty M Gumbo , Wah. Madiwani , Mkuu wa wilaya Mhe. Faiza Salim na wataalamu ilisimamia mchakato wa ukopeshaji vikundi 20 vya wanawake kiasi cha Tshs. Milioni 53,979,246/, vikundi 20 vya Vijana vilikopeshwa kiasi cha Tsh . Milioni 37,520,754/- na vikundi 8 vya jamii ya watu wenye ulemavu kiasi cha Tsh. Milioni 32/- na kiwa jumla ya Tsh. Milioni 123,500,500/- Kwa vikundi vyote.
Hivyo basi kwa mwaka wa fedha mpya wa 2022-2023 Halmashauri imepangiwa kukusanya kiasi cha Tsh Bilioni 1,635,700,000/- ni ongezeko la asilimia 10(%) kutoka kwenye bajeti ya 2021 - 2022.
Nini maana ya makusanyo haya kikanuni na kimiongozo kiasi cha asilimia 40 (%) kitarudi Kwa wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo na kusogeza huduma muhimu karibu na Wananchi kama Elimu, Afya, maji, umeme na miundombinu ya barabara na asilimia 10 (%) itatumika katika kuibua wajasiliamali wapya kwa kuwawezesha wananwake , Vijana na walemavu.
Kwa mantiki hiyo wanaitilima tunakwenda kuijenga itilima yeti wenyewe kupitia makusanyo yetu ya mapato ya ndani ni vyema zaidi tukawa kitu kimoja katika kuijenga itilima Kwa kutimiza wajibu wa kisheria na Kikanuni.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa