Mwenyekiti wa Tume Taifa ya Uchuguzi Jaji, Semistocles Kaijage amezindua mafunzo maalumu kwa ajili ya uboreshaji wa daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwa Maafisa Uchaguzi ngazi ya Kata (ARO) Wilayani Itilima.
Akiwa Wilayani humo Mhe. Jaji Kaijage alisema "Mnapaswa kufuatilia mafunzo haya kwa umakini ili Itilima iwe miongoni kwa Wilaya ambazo zitafanya vizuri Nchini katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpigakura"
Aidha, Msimamizi wa Shughuli za Uchaguzi Mkoa Ndg. Saimon Maganga aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha wanafuatilia mafunzo kwa lengo la kutekeleza kwa ufanisi zoezi hili la Kitaifa la Uboreshaji wa daftari la Kudumu la Mpiga la kura.
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga kura limezinduliwa Nchini hivi karibuni na kwa Itilima uandikishaji utaanza rasmi tarehe 31/07/2019 kwa lengo la kujianda na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa hapo Mwezi Oktoba mwaka huu na Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwaka 2020.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa