HAKIKISHENI MNAWAPELEKA WATOTO WENU KUPATA CHANJO YA SURUA NA LUBELLA: MKUU WA WILAYA YA ITILIMA
Mkuu wa wilaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi Leo amezindua Kampeni ya Siku tano ya chanjo ya Surua na Lubella katika viwanja vya Zahanati ya Lagangabilili wilayani Itilima.
Akizindua Kampeni hiyo kwa niyaba ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Katibu tawala (W) Itilima Mhe. Filbert Kanyilizu alisema
"Itilima inakusudia kuwapatia chanjo ya Surua na Lubella watoto wapao 88,555 wenye umri wa miezi 9 mpaka miezi 59 na chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri wa Mwaka Mmoja na nusu mpaka miaka mitatu na nusu"
Vilevile Katibu tawala huyo aliwaasa Wananchi hao kuto puuza zoezi hilo la chanjo kwani husaidia watoto kuepukana na Udumavu wa afya ya akili na mwili.
Akiongea na wananchi waliyoudhuria katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya chanjo ya Surua na Lubella Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (W) Itilima Bi. Elizabeth Gumbo alisema.
"Wakina Mama wenzangu hakikisheni mnawapeleka watoto wenu katika vituo vya kutolea huduma ya afya kupata chanjo hii na mpeleke elimu hii kwa majirani zenu ili nao watoto wao wapate huduma hii kwani bila kufanya hivyo hatutaweza kuzuia mlipuko wa maambukizi katika maeneo yetu"
Aidha Bi. Gumbo aliwaasa wananchi kuachana na fikra potofu ya kwamba chanjo hiyo itawaletea athari watoto wao hususani katika afya ya uzazi au kusababisha kifo kwa watoto wao.
Kampeni hii ya chanjo Surua na Lubella imezinduliwa rasmi leo na Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na zoezi hili litafanyika Mikoa yote ya Tanzania bara na kuhitimishwa rasmi tarehe Oktoba 21, 2019.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa