Na. Haruna Taratibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Bi. Elizabeth Gumbo siku ya Jumatatu ya tarehe 31 Oktoba 2022 ameingia Mkataba na Maafisa Watendaji wa Kata zote 22 za Wilaya ya Itilima Kwa ajili ya utekelezaji na ufuatiliaji wa Afua za Lishe wilayani humo.
Bi. Gumbo alisema ya kwamba tunaingia hii mikataba ya kiutekelezaji Ili kuleta ufanisi katika lishe na ikitokea Mtendaji yoyote kuzembea na kutotimiza wajibu wake Mkataba huu utatumika kama kielelezo katika kuwajibika.
Akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Itilima katibu Tawala Ndg. Filbert Kanyirizu alitoa wito Kwa Watendaji wa Kata kuifanya Lishe kuwa Ajenda ya kudumu katika vikao vyao vya Kata (WADC) na aliwaomba Viongozi wa dini kutoa elimu Kwa waumini wao kuhusiana na lishe.
Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Anold Musiba alibainisha umuhimu wa ufuatiliaji wa Afua za Lishe katika wilaya ya Itilima na Moja ya vigezo Tisa vinavyo takiwa kutekelezwa ni pamoja na kuwa na Vikao vya kujadili hali ya lishe kwa kila robo.
Afisa Lishe wa Wilaya ya Itilima Ndg. Oswin Mlelwa alibainisha hali ya lishe Kwa wilaya ya Itilima ikiwemo upatikanaji wa Vitamini A Kwa mwezi Januari - Machi ulikua 66%, mwezi Aprili - June ulikuwa 136% na June - Septemba ulikuwa 47%.
Aidha Afisa Lishe alibainisha ya Kuwa Halmashauri ya Itilima imetenga vituo 11 vitakavyo hudumia watoto wenye utapiamlo mkali na Kila kituo kimewekewa utaratibu wa kuhudumia watoto 10.
Vituo hivyo ni Chinamili kimehudumia watoto 4 waliyopokelewa, Sagata watoto 6, Migato watoto 5, Lagangabilili watoto 5, Luguru watoto 6, Nangale watoto 4, Mahembe watoto 8, Zagayu watoto 3, Nkoma watoto 16, na Mwamapalala watoto 5.
Aidha, Afisa Lishe aliwasisitiza Watendaji wa Kata waende kuwasisitiza Wahudumu wa Afya kuwatembelea Wajawazito majumbani Ili kugundua kama Wana dalili za hatari na wakijifungua wasisitizwe kunyonyesha watoto Maziwa ya Mwanzo ni muhimu Kwa Kinga ya asili ya Mtoto.
Ilisisitizwa muda wa Mtoto kunyonya ni Miezi sita bila kuchanganyiwa na chakula kingine na miezi sita hiyo ni sehemu ya siku 1000 muhimu Kwa makuzi ya kimwili na kiakili ya Mtoto.
Katika Majadiliano, Mtendaji wa Kata ya Mwamapalala Ndg. Samwel ambaye Kata yake ni miongoni mwa zilizo fanya vizuri, alishauri kuwa, wahudumu wa Afya wanafanya kazi kubwa sana kuwatembelea wananchi, basi wawe wanaangaliwa Kwa jicho lingine la uwezesho Ili kiwapa moyo na tufikie malengo.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa