MKUU WA Wilaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi awataka viongozi wote wa Vyama vya Msingi (AMCOS) kuhakikisha wanawasaidia Wakulima na si kujielekeza kwenye maslahi binafsi na kumuuacha mkulima akikata tamaa kujihusisha na zao la pamba.
Akiongea na wadau wa zao la Pamba katika kikao cha maandalizi ya Msimu mpya wa kilimo wilayani Itilima, na mapitio ya changamoto zilizo jitokeza msimu uliyo pita, Mhe. kilangi alisema '' dhamana ya Viongozi wa Amcos ni kuwasaidia wakulina na kuhakikisha zao la pamba linaimarika na si vinginevyo na sitaki kusikia kiongozi wa Amcos ni Mtuhumiwa, ukishatuhumiwa unatakiwa ujiuzuru''
Kauli hiyo ya Mkuu wa Wilaya imekuja baada ya malalamiko ya Wadau wa zao la Pamba kwa baadhi ya viongozi wa Amcos kutokuwa waaminifu kwa makampuni na kwa wanachama wao.
Akithibitisha uwepo wa tuhuma dhidi ya Viongozi wa Amcos Mkuu wa Kituo cha Polisi Lagangabilili, OCS Bwire alisema
“tumepokea malalamiko kutoka kwa Wanachama wa Amcos kuwa viongozi wao hususani Makatibu wanatumia pesa za wanachama kienyeji na kusingizia zimepotea, tutafanya uchunguzi tukibaini upotevu ni wa kizembe watawajibika”
Hata hivyo Mhe. Kilangi alitoa agizo kwa kamanda wa Polisi Wilaya (OCD) kuhakikisha anawakamata viongozi wote wa Amcos waliyo hujumu pesa za Wanachama na Makampuni.
Akiongelea Ukopeshaji wa Mbegu za Pamba kwa wakulima, kwa Msimu mpya wa Kilimo, Mhe. Mkuu wa wilaya alimtaka Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Ndg. Kelisa Wambula kuhakikisha kupitia Watendaji wa Vijiji wapeleke taarifa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya majina yote ya Wakulima waliyo pata mbegu na maeneo yao ya Mashamba.
Agizo hilo la Mkuu wa Wilaya limekuja baada ya Maelezo ya Mkaguzi wa Pamba wilaya Ndg. Said Itaso kulalamikia zoezi la ugawaji wa mbegu za Pamba kwa baadhi ya Maeneo kutokuwa na uaminifu baada ya kugawa kwa kutumia Mzani, viongozi wa Amcos wanatumia Makopo kupimia mbegu hizo.
Aidha Mkaguzi huyo wa Pamba alisema kuna baadhi ya makampuni yamekiuka makubaliano ya kuziwekea Mbegu sumu kali, lakini cha kusikitisha wameweka sumu chache, matokeo ya baadae mbegu zinaweza zisikabiliane na wadudu waharibifu.
Bw. Itaso aliomba elimu iendelee kutolewa kwa Wakulima kusafisha masalia ya pamba
Katika mashamba yao ili kupunguza magonjwa na masalia ya waduu wanao baki katika masalia hayo. Vile vile alitoa elimu ya kuandaa dawa ya kukabiliana na unyaukaji wa majani kwa kuchanganya sabuni ya unga kilo moja na mafuta ya kula lita moja , ukipatikana mchanganyiko wa sabuni na mafuta unachanganywa na lita 150 za maji, mchanganyiko huu unatibu magonjwa yanayo ikabili pamba.
Msimu mpya wa kilimo umeanza na Serikali kupitia Bodi ya pamba wameipatia Wilaya ya Itilima tani 1400 za mbegu ya pamba ili wakulima wakopeshe, ingawa kuna changamoto ya kuto tosha kwa mbegu hizo. Msimu wa mwaka huu Wilaya ya Itilima iliweza kuvuna Pamba kiasi cha kilo milioni 18 na mwaka jana ilivuna kilo milioni 11.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa