Na. Haruna Taratibu
Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Faidha S. Salim amewaasa wataalamu kutimiza wajibu wao katika utekelezaji wa Miradi ya maendeleo, hususani miradi inayoletewa fedha Kulingana na matokeo utekelezaji.
Akiwa katika ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Tasaf Mhe. Faidha alisema
"Waratibu wa Tasaf wanapaswa kujitathmini kutokana na miradi inavyo sua sua, mafundi kutosimamiwa inavyo takiwa na vifaa vya ujenzi kutokuwepo katika eneo la mradi"
Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Faidha Salim aliyevaa Kofia akikagua Madarasa katika Mradi wa shule ya sekondari Nhobora ambapo shule hiyo ilitengewa kiasi cha Tshs. Milioni 470/ za utekelezaji |
Mhe. Faidha alitembelea Mradi wa Bweni la wanafunzi wa Kike katika Kijiji Cha shishani ambapo Mradi huo upo katika hatua ya Upauaji.
Katika Mradi wa Shule ya Sekondari Nguno ambapo umeanza na ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa ofisi na Vyoo Mhe. Mkuu wa wilaya alishauri kurekebishwa Kwa baadhi ya Kasoro zilizo onekana katika umaliziaji hususani katika Mikanda inayoshikilia (gypsum board) na kuwaelekeza wataalamu kuwaonesha wananchi sehemu sahihi ya kuweka vifaa vya ujenzi kama mawe na Mchanga ili kusijitokeze hamisha hamisha ya malighafi hizo za ujenzi baada ya kuletwa
Mkuu wa wilaya ya Itilima Mhe. Faidha Salimu akikagua miundombinu katika jengo la Dharula la Hospitali ya Wilaya ya Itilima. |
Mhe. Mkuu wa wilaya na kamati yake ya ulinzi na usalama walifanya ziara katika miradi ya Tasaf, kituo Cha Afya Kanadi, Hospitali ya Wilaya na Shule ya Sekondari ya Nhobora miradi yote hiyo ina thamani ya zaidi ya Tshs. Bilioni 2.17.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa