Na. harunataratibu82@gmail.com
Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri (Wilaya) Itilima kwa mwaka wa fedha 2021 - 2022 umebariki kwa kauli Moja Mabadiliko ya Matumizi ya Fedha kiasi Cha Sh. Milioni 400 kilichokuwa kitumike katika muendelezo wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
Hivyo Wah. Madiwani waliona ni vyema Fedha zikaenda kukamilisha ujenzi wa Zahanati tatu za Dasina, Nhobora na Laini na maboma ya Vyumba vya Madarasa kwa Shule za Msingi, pamoja na Ujenzi wa nyumba mbili za Watumishi Moja ikijengwa katika Hospitali ya Wilaya.
Akifunga mjadala wa hoja hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri (W) Itilima Mhe. Daudi Nyalamu alitoa mchanganuo utakao ongoza matumizi ya Fedha hizo, kuwa kiasi cha Sh. Milioni 300 kitatumika katika ukamilishaji wa Zahanati tatu na maboma ya Madarasa kwa Shule za Msingi na Sh. Milioni 100/ itatumika katika ujenzi wa Nyumba mbili za Watumishi Moja itajengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Itilima.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa