Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Bilioni 9.6
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Itilima katika mkutano wake maalumu wa Baraza leo Februari 14, 2020 limejadili na kuidhinisha kwa kauli moja bajeti yake ya Tshs 28, 536,837,339/- kwa mwaka wa fedha 2020/2021
Ambapo Tshs. 1,434,558,653 ni mapato ya ndani ya Halmashauri na Tsh. 1,472,997,839/- ni Mapato ya Ruzuku kutoka Serikali kuu, zikijumuisha Tshs. 21,704,337,000/- kwa ajili ya mishahara na Tshs 3,924,943,847 ni Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo.
Akizungumza wakati wakupitisha bajeti hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Daudi Nyalamo amebainisha kuwa
“ili kuwa na dira na kufikia malengo chanya, Halmashauri imeandaa mpango wa mwaka 2020/2021 na Mpango wa muda wa kati 2020/2021-2022/2023 unaolenga kukuza uchumi na kupunguza umaskini na kufikia maendeleo endelevu, ya Kijamii, Kiuchumi na Kimazingira kwa wananchi wake”.
Aidha Mhe. Mwenyekiti aliwaomba Wajumbe kujikita kwenye Mpango huo ambao umeshajadiliwa katika mabaraza mbalimbali ikiwemo Baraza la Wafanyakazi, Kikao cha Ushauri cha Wilaya (DCC) na Kamati ya fedha Utawala na Mipango.
Vipaumbele vya mpango huo uliyo wasilishwa na Afisa Mipango na Ufuatiliaji Ndg. Paulo A. Nyalaja kwa niyaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (W) Itilima Bi. Elizabeth M. Gumbo Umelenga yafuatayo.
kuboresha na kuimarisha ukusanyaji wa Mapato ya ndani kwa kuongeza mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato (POS) ili kudhibiti upotevu wa Mapato, kuendeleza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ili ikamilike kwa kiwango kinacho kubalika na kuanza kutoa huduma mapema iwezekanavyo, kukamilisha madarasa kwa shule za msingi na Sekondari na kuanza kutumika ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia na ukamilishaji wa jengo la utawala.
Miradi ya iliyotengewa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri katika mwaka wa fedha 2020/2021 ni ukamilishaji wa ujenzi wa Zahanati ya Bulolambeshi, Zahanati ya Laini, Zahanati ya Mbogo, Zahanati ya Songambele, Zahanati ya Nkololo na Zahanati ya Kidula kwa Tsh. 213,995,599.98/-
Miradi ya elimu iliyo tengewa Fedha ni Ukamilishaji wa Bweni katika shule ya sekondari Lagangabilili ifikapo juni 2021 kwa Tsh. 45,000,000/- pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba za walimu 3 katika shule 3 za msingi kwa Tsh. 58,995,746/-
Miradi ya ardhi iliyo tengewa fedha ni pamoja na kulipa fidia na kupima maeneo muhimu kwa ajili ya ujenzi wa Viwanda, Soko na eneo la Maziko.
Diwani wa Kata Zagayu Mhe. Wiliamu Kuzenza akichangia mada katika kikao cha Baraza maalumu la bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
|
Rasimu ya Mapendekezo ya Bajeti ya Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) ya kiasi cha Tsh. Milioni 623.18/ iliyo wasilishwa na Mhandisi Athumani Bakari kwa niyaba ya Meneja wa Tarura Wilaya ya Itilima Mhandisi Chinengo, S.N.Y ililigawa baraza hilo kutokana na hali ya sasa ya uharibifu mkubwa wa mtandao wa Barabara uliyo sababishwa na mvua za vuli kupelekea sehemu kubwa ya Wilaya kutopitika.
Ushauri uliyo tolewa na Baraza kwa Tarura ni kuhakikisha wanakuwa na utaratibu wa kujenga barabara moja na kuikamilisha na kwenda nyingine na kuachana na mfumo wao wasasa wa kutengeneza kila mahali wakijua bajeti yao ni finyu.
Hata hivyo Wakala kwa Itilima umewasilisha maombi ya Fedha za matengenezo kiasi cha Tsh. Milioni 317 kwa Mtendaji Mkuu TARURA ili kukarabati maeneo yaliyo athirika na Mvua za Vuli.
Wahe. Madiwani wakiwa katika kikao cha Baraza maalumu la bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
|
Aidha kwa upande wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wamewasilisha mapendekezo ya bajeti ya Maji kwa ujumla kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kiasi cha Tsh. Bilioni 9.6 kwa mchanganuo ufuatao
Bajeti ya Miradi inayo endelea itakamilishwa na kuanza kutoa huduma kwa Tsh. Bilioni 3, Miradi ya Ukarabati Wakala uanataraji kutumia Tsh. Milioni 60, Miradi ya upanuzi ili kusogeza huduma kwa Wananchi wakala utatumia Tsh. Bilioni 1.9, Miradi mipya Wakala umepanga kutumia Tsh. Bilioni 4.6, uendeshaji wa ofisi na stahiki za Watumishi Wakala umepanga kutumia Tsh. Milioni 69.
Miradi mipya iliyo pangwa kutekelezwa na Wakala katika bajeti ya 2020/2021 ni Mradi wa Maji Habiya ambao utahusisha vijiji 6 vya Mwazimbi, Bulolambeshi, Bumera, Habiya, Gaswa na Mwandulu na kuhudumia kuhudumia watu 18,361 chanzo chake ikiwa ni bwawa la Habiya, bajeti iliyo kadiliwa kugharamia mradi huu Tsh bilioni 4 na Mradi wa Maji katika kijiji cha Ng’esha ambao utahudumia watu 3,437 na bajeti iliyo kadiriwa kugharamia mradi huu ni Tsh. 650,000,000/-
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa