TAARIFA YA MIRADI ILIYOTEKELEZWA WILAYANI ITILIMA KWA NJIA YA PICHA KWA MWAKA WA FEDHA
(2016/2017 2017/2018)
Mradi wa Usambazaji Maji Katika Kijiji cha Lagangabilili
Mradi Wa Usambazaji Maji Katika Kijiji cha Lagangabilili Wenye Thamani ya
Tsh. 907,617,866, Fedha Zote Zimetoka Serikali Kuu. Picha Ya Kwanza Inaonesha Tanki la Maji, Kituo cha Kuchotea Maji na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu. Charles Francis Kabeho Akizindua Mradi.
Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za Afya katika Kituo cha Afya Ikindilo
Uboreshaji wa Huduma za Afya Katika Kituo cha Afya Ikindilo kwa Tsh. 525,000,000 unaendelea kutekelezwa kwa ukamilishaji wa Jengo la Maabara, Jengo la kuhifadhia Maiti, Mtandao na Maji. Aidha, Jengo la Upasuaji, Wodi ya Wazazi na Nyumba ya Mtumishi Imekamilika.
Wodi ya Uzazi Katika Zahanati ya Migato Imejengwa kwa Tsh. 30,000,000 ni Moja Kati ya Wodi 5 Zilizojengwa kwa Jumla ya Tsh. 150,000,000 chini ya ufadhili wa UNFPA
Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu
Ujenzi wa Madarasa 4 na Ununuzi wa Madawati Katika Shule ya Msingi Lagangabilili
kwa Thamani ya Tsh. 80,000,000 Kupitia Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo (P4R) umekamilika.
Ujenzi Wa Vyumba 3 vya Maabara za Masomo ya Sayansi Katika Shule ya Sekondari Budalabujiga kwa Thamani ya Tsh. 125,767,000.
Wanafunzi wa Masomo ya Sayansi Katika Shule ya Sekondari Budalabujiga Wakiendelea na Mafunzo kwa Vitendo (Practical).
Ujenzi wa Mabweni 2 Katika Shule ya Sekondari Itilima kwa Thamani ya Tsh. 293,200,000 Yenye Uwezo wa Kubeba Wanafunzi 240 fedha zote zimetoka Serikali Kuu.
Ujenzi wa Bweni Jipya la Wanafunzi wa Kike Katika Shule ya Sekondari Nkoma Chini ya Ufadhili wa Ubalozi wa China kwa Thamani ya Tsh.178,448,000 Lenye Uwezo wa Kubeba Wanafunzi 160.
Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji
Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Itilima Ukiwa Umekamilika kwa Awamu ya Kwanza kwa Thamani ya Tsh. 670,590,194 Ukiwa Umejumuisha Mifumo ya Maji Safi, Maji Taka na Umeme.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa