Saturday 18th, January 2025
@
Mkuu wa Wilaaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi, katikati mwenye jaketi la Bluu akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya Madiwani wenye jezi ya njano na kijani na timu ya watumishi wenye jezi nyekundu
|
Maadhimisho ya Kumbukizi ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere yalihitimishwa wilayani Itilima na mechi Kali baina ya Madiwani wa Halmashauri (W) Itilima na Watumishi wa Halmashauri hiyo.
Mtanange huo uliyofanyika katika Viwanja vya shule ya Msingi Lagangabilili ulimalizika kwa timu ya Madiwani Kubugizwa magoli 2-1.
Kipindi cha kwanza cha Mtanange huo kilimalizika kwa Kikosi cha Watumishi kuongoza kwa goli moja kwa nunge ambapo timu ya Madiwani ilijifunga baada ya kutokea piga nikupige katika lango la timu ya madiwani iliyokuwa ikiongozwa na Nahodha wao Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe. Njalu D. Silanga.
Goli la pili lilipatikana katika kipindi cha pili na liliwekwa kimiani na Mweka hazina wa halmashauri hiyo ndugu salmin ambaye aliichachafya vikali ngome ya timu ya Waheshimiwa Madiwani.
Bao la kufutia Machozi la kikosi cha Waheshimiwa Madiwani Liliwekwa Kimiani kwa Mkwaju wa Penati na Mshambuliaji Machachali Mhe. Robert Jongela baada ya beki wa timu ya Watumishi kumchezea ndivyo sivyo Mshamuliaji hatari wa Madiwani, ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Daudi Nyalamo na Mwamuzi wa Mchezo huo kuamua Ipigwe penati.
Mpaka mwisho wa Mchezo huo timu ya Watumishi ilifanikiwa kuondoka na alama zote tatu na magoli mawili.
Kwa upande wa Mpira wa pete, ulizikutanisha timu ya Wanawake ya Watumishi na Madiwani Wanawake na Mchezo kumalizika kwa timu ya Watumishi kuchakazwa kwa Alama 5-1.
Mechi zote mbili zilishuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi na Mkurugenzi wa Halmashauri (W)Itilima Bi. Elizabeth Gimbo.
|
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa