Mandhari ya Mji wa Lagangabilili ambao ni makao Makuu ya Wilaya ya Itilima, yamekua yakibadirika Kwa Kasi baada kutengewa fedha kiasi Cha Milioni 500/- kwa ajili ya ujenzi wa kilomita Moja ya barabara kwa kiwango cha Lami na zoezi la ufungaji wa taa za pembezoni mwa barabara likiwa linaendelea.
Mkandarasii anaye tekeleza mradi huo, kampuni ya M/S Civmark limited ya Dar - es - Salaam mapema mwaka huu iliingia Mkataba na Tarura Mkoa wa Simiyu wenye thamani ya Tsh. Milioni 499.9 wa ujenzi wa Barabara yenye urefu wa Kilometa 1.2 na ufugaji wa taa za pembeoni mwa barabara, uwekaji wa makalavati na mitalo ya kusafirishia Maji ya mvua
Itilima ni miongoni mwa Wilaya mpya ambayo serikali ya awamu ya sita imeshawekeza kwenye miradi tofautitofauti yenye thamani ya zaidi ya Tshs. Bilioni 40/- ikiwemo huu mradi wa barabara wenye thamani ya Tsh. Milioni 500.
DED - ITILIMA
Sanduku la Posta: 308 BARIADI
Simu: +255 28 29 863 29
Simu: 028 29 863 28
Barua Pepe: info@itilimadc.go.tz
Hatimiliki ©2016 Kitengo cha TEHAMA. Haki Zote Zimehifadhiwa